Na Mwandidhi wa EANA
Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesisitiza
kuendeleza ushirikiano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwani amesema ni
moja ya nguzo muhimu katika kipindi cha utawala wake.
''Lengo letu kuu katika kuimarisha biashara na
uwekezaji utakuwa ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla,''
Rais Kenyatta alinukuliwa akisema alipokutana na Katibu Mkuu wa EAC, Dk Richard
Sezibera aliyekwenda kumtembelea ofisini kwake mjini Nairobi
Juzi.
Aliongeza kuwa kuondolewa kwa vikwazo vya biashara
kupewe kipaumbele kadiri mtangamano wa EAC unavyozidi kuimarika na kupanuka,
Shirikia Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA)
limeripoti.
''Kuondolewa kwa vikwazo vya kazi na kusafiri kwa
raia ndani ya nchi wanachama kutasaidia zaidi kukua kwa biashara na
kubadilishana mawazo,'' alisema Rais Kenyatta.
''Tunaweza kufanya vizuri zaidi tukiwa katika kanda
kuliko nchi mojamoja,'' aliongeza Rais.
Naye Katibu Mkuu wa EAC, Dk Sezibera alimpongza Rais
kwa kushinda uchaguzi wa rais hivi karibuni na kuwashukuru pia wananchi wa Kenya
kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa jinsi walivyoendesha uchaguzi
huo.
Post a Comment