Waandishi wa habari wanachama wa APC wakifuatilia kwa makini mkutano wa dharura ulioitishwa na chama hicho, kushoto ni Daniel Sabuni, Cynthia Mwilolezi na Janeth Mushi
*******
|
Akizungumza mapema leo kwenye kikao cha dharula kilichokuwa na lengo ya kupanga siku ya uchaguzi ambayo imekubaliwa kuwa ni Juni Mosi,mwaka huu,Mwenyekiti wa APC,Claud Gwandu alisema ameita kikao hicho ili kuomba ridhaa ya wananchama kupanga tarehe ya mkutano mkuu na uchaguzi kutokana na kukabiliwa na maandalizi ya siku ya vyombo vya habari itakayofanyika katika ngazi ya Kanda kwenye jiji la Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 200.
Alisema kikatiba uchaguzi ulitakiwa kufanyika mwezi Mei lakini kutokana na kuwa APC ndio wenyeji wa siku ya vyombo vya habari imeonekana ni busara kusogeza mbele siku ya mkutano mkuu ambayo itaenda sanjari na kufanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa APC.
Kikao hicho kimewapitisha wajumbe watano watakaosimamia uchaguzi huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na kila mwanachama kuamini ana uwezo wa kuongoza akishirikiana na wanachama wenzake.
Katibu wa APC,Eliya Mbonea alisema mchakato wa kuandaa fomu zitakazotumwa kwa wanachama utafanywa na kamati ya uchaguzi ambayo wajumbe wake ni waandishi wakongwe,Willam Lobulu,Danford Mpumilwa,Mch Amos Sekajingo,Zephania Ubwani na Kulwa Mayombi.
Baadhi ya wanachama waliozungumza na Blog hii hawakupenda kutaja nafasi watakazowania kuwa ni mapema mno kutangaza na ni moja ya mbinu za kisayansi kusaka ushindi.
Uongozi unaomaliza muda wake unajivunia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na kuwa na ofisi ya kudumu,mafunzo ya mara kwa mara,vitendea kazi na baadhi ya wanachama kulipa ada kwa wakati.
MAJADILIANO: Mratibu wa APC, Seif Mangwangi wa pili kutoka kulia, Katibu wa APC Eliya Mbonea, mwanachama Richard Konga na Bertha Ismail wa kwanza kulia wakijadili jambo |
Makamu Mwenyekiti wa APC, Charles Ngereza pamoja na Anthony Masai wakionyeshana jambo kwenye komputa
JAMIIBLOG
|
Post a Comment