Mheshimiwa Angellah
Kairuki(MB),Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akiwa namwenyeji wake Mhe.Sayid
Ashraful Islam, Waziri wa Serikali za Mitaa Maendeleo Vijijini na
Ushirika(Wizara inayoshughulika na Usajili wa Vizazi naVifo)wakati wa ziara yake
nchini Bangladesh kujifunza namna ambavyo nchi hiyo imewezakufikiaa silimia
zaidi ya 95 ya usajili wa Vizazi
naVifo.
Mheshimiwa Angellah
Kairuki, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akijibu baadhi ya maswali ya waandishi
wa habari wa Bangladesh
Mheshimiwa Angellah Kairuki akifafanua jambo kwa Mhe.Mhe.
Hassanul Haq Inu, Waziri wa Habari wa Bangladesh wakati wawili hao walipokuwa
wakisubiri kukutana na waandishi wa habari wa Bangladesh na kueleza madhumuni ya
ujumbe wa Tanzania kwenda nchini Bangladesh kujifunza namna ya kuboresha mfumo
wa usajili wa vizazi na vifo hadi kufikia asilimia mia moja (100%).
Mhe.
Angellah Kairuki akielezwa jambo na Bw. Nazrul Islam, Mtendaji Mkuu wa Dhaka
South City Corporation
Mhe.
Angellah Kairuki katika picha ya pamo jana Sir. Fazle Abed, Mwanzilishi na
Mwenyekiti wa taasisi ya BRAC alipotembelea Makao Makuu ya
BRAC.
Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake wa
wataalam kutoka Taasisiza RITA, NIDA, TRA, Serikali zaMitaa, e-Government,
Tumeya Taifaya Uchaguzina Ofisi ya Takwimu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Wenyeji wake.
----
USAJILI WA
VIZAZI NA VIFO NCHINI
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa
Angellah Kairuki aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenda nchini Bangladesh
tarehe 5-11 Aprili 2013.
Ujumbe
huo uliojumuisha wataalam kutoka taasisi mbalimbali za Serikali zinazojihusihana
masuala ya usajili ikiwa ni pamoja na RITA,
NIDA, TRA, Serikali za Mitaa,
e-Government,
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi na Ofisi ya Takwimu ulikwenda kujifunza namna ambavyo nchi ya Bangladesh ilivyoweza
kufanikiwa katika zoezi la Usajili wa Vizazi naVifo kwa zaidi ya asilimia 95 ya
wananchi wao.
Katika
ziara hiyo Mheshimiwa Naibu Waziri na ujumbe wake walijionea jinsi ambavyo zaidi
ya huduma 16 muhimu nchini Bangladesh zilivyounganishwa na Mfumo wa kusajili
vizazi na vifo na umuhimu wa cheti cha
kuzaliwa.
Huduma
hizo ni pamoja naVitambulisho vya Taifa, Leseni ya Biashara, Kitambulisho cha
mlipa Kodi (TIN), leseni ya kuendesh agari, hati ya kusafiria, leseni ya
ukandarasi, vibali vya ujenzi, leseni ya kusafirisha na kuagiza bidhaa ndani na
nje ya nchi, kuunganishi wa huduma muhimu kama umeme, maji, simu n.k. bila kuwa
na cheti cha kuzaliwa mwananchi wa Bangladesh hawezi kupata huduma moja wapo
kati ya hizo.
Serikali kwa kutambua
umuhimu na faida za kusajili vizazi na vifo,imedhamiria kuboresha mfumo wa
Usajili na kunyanyua kiwango cha Usajili kwa kuanzisha Mpango wa Usajili wa
Watoto wote walio na umri chini yaMiaka Mitano (Under Five Birth Registration
Initiative(U5BRI) na mpango wa usajili wa watoto wenye umri wa miaka
6-18.
Katika
mpango huu waUsajili,mtoto atasajiliwa na kupatiwa cheti papohapo, na hivyo
kufanya zoezi zima la usajili kuwa la hatua moja badala ya hatua mbili
zinazotumika sasa, yaani kusajili kwanza kisha kupata cheti baadaye. Pia Mpango
huu unalengo la kugatua madaraka ya shughuli za usajili kutoa Serikali Kuu na
kupeleka katika Serikali za Mitaa na Vituo vya
Afya.
Post a Comment