Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Vituo saba vya afya Singida vyapokea msaada vya vitanda maalum vya kujifungulia akinamama kutoka PSI.

 

Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la PSI-Tanzania kanda ya kati, Zena Mgoi (wa kwanza mbele) akitoa nasaha zake muda mfupi kabla hajakabidhi msaada wa kitanda cha kujifungulia akina mama wajawazito kwa zahanati ya Tumanini Singida mjini.
Mratibu wa afya ya uzazi wa shirika la PSI, Zena Mgoi (kulia) akimkabidhi mkurugenzi wa zahanati ya Tumaini Dk. Halvin Mlay msaada wa kitanda cha kujifungulia akina mama wajawazito.
Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Joseph Malunda (wa kwanza kulia) akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa kitanda cha kujifungulia kilichotolewa kwa zahanati ya Tumaini iliyopo mjini Singida.
Mkurugenzi wa zahanati ya Tumaini iliyopo mjini Singida, Dk.Halvin Mlay akitoa shukurani zake kwa msaada wa kitanda cha kujifungulia akina mama wajawazito katika zahanati yake.Aliyeketi ni Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Joseph Malunda.
Jengo la zahanati ya Tumaini iliyopo mjini Singida.Aliye mbele ya jengo hilo ni mmiliki wa zahanati hiyo.(Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu wa Mo Blog
Shirika lisilo la kiserikali la PSI-Tanzania kanda ya kati, limetoa msaada wa vitanda saba maalum kwa ajili ya kujifungulia akina mama wajawazito kwa zahanati na vituo vya afya saba mkoani Singida,vyenye thamani ya zaidi ya Sh.6 milioni.
Zahanati na vituo vya afya vilivyonufaika na msaada huo ni Isanzu, Kinampanda, Lambi zahanati na Iambi hospital vyote vya wilaya mpya ya Mkalama.
Vingine ni Sepuka, Tumaini na polisi, vyote vya wilaya ya Singida.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo, mratibu wa afya ya uzazi wa PSI Zena Mgoi, amesema msaada huo umetolewa na shirika lao, ikiwa ni zawadi kwa kazi nzuri ya kutoa huduma bora ya afya ya mama na mtoto kuanzia mwaka jana hadi sasa.
Zena amesema ushirikiano mzuri kati ya PSI-Tanzania na vituo hivyo, umechangia kuleta matokeo mazuri katika kutoa huduma mbalimbali bora ikiwemo uzazi wa mpango.
Aidha, Zena ametumia fursa hiyo kutoa ahadi kwamba PSI-Tanzania itaendelea kushirikiana na kutoa misaada mbalimbali ili kuboresha utoaji wa huduma bora za afya ikiwemo ya mama na mtoto.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa zahanati ya Tumaini Dk.Halvin Mlay, amelishukuru shitrika la PSI-Tanzania kwa ushirikiano linaoutoa kwa vituo vya afya na zahanati mkoani Singida.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top