Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAUZO YA MAZAO YA SAMAKI YAINGIZA SHILINGI BILIONI 54.4 NCHINI TOKA 2005 HADI 2012



Bunge-TanzaniaNa Benedict Liwenga, Maelezo, Dodoma.
 
Jumla shilingi bilioni 54.4 zimepatikana zimepatikana kutokana na ushuru kwa mauzo ya mazao ya samaki hapa nchini.
Takwimu hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Benedict Ngalama Ole-Nangoro wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Wawi, Mhe. Hamad Rashid Mohamed aliyetaka kujua katika kipindi cha mwaka 2005 hadi2012 Tanzania imesafirisha tani ngapi za mazao ya Samaki kutoka Bahari Kuu na Maji baridi (Maziwa), na Meli ngapi za uvuvi wa Bahari Kuu zilipewa leseni na zilisafirisha tani ngapi za Samaki kwa thamani gani na je Serikali imepata mapato kiasi gani kwa kutoza kodi za aina gani.
Amesema kati ya mapato hayo shilingi bilioni 5.5 ni kutoka maji chumvi na bilioni 48.9 zilitokana na samaki wa ziwani au maji baridi.
Mhe. Ole-Nangoro amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012, Tanzania imesafirisha jumla ya tani 371,317.8 za samaki na mazao ya uvuvi ambapo tani 17,954.5 ni kutoka maji chumvi na tani 353,362.7 kutoka maji baridi ambapo Ziwa Victoria ni 339,893.1, Tanganyika 11,418.8, Nyasa 110.9 na maeneo ya maji madogo ni 1,939.9 pamoja na Samaki hai 301,839.
Aidha, ameongeza kuwa kati ya mwaka 2005 hadi 2009, jumla ya leseni 274 zilitolewa na Tanzania bara kwa ajili ya uvuvi katika bahari kuu.
“Kabla ya mwaka 2009, wakati Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu kuanzishwa, Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar zilikuwa zinatoa leseni kila mmoja kwa ajili ya uvuvi katika bahari kuu”. Mhe. Ole-Nangoro alisema.
Amesema kuwa baada ya kuanzishwa Mamlaka hiyo, kati ya mwaka 2010 hadi 2012 jumla ya leseni 124 zilitolewa.
Aidha , Naibu Waziri huyo amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012 jumla ya meli 398 zilipewa leseni za uvuvi wa Bahari Kuu, ambapo Meli zote zilizopewa leseni hizo zilivua jumla ya tani 40,081.8 za samaki ambazo zilisafirishwa na kuuzwa nje ya nchi.
Katika hatua nyingine Serikali imesema kuwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012 ,jumla ya shilingi bilioni 12.6 zimepatikana kutokana na ada ya leseni .
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top