Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwan Athuman. |
Mgogoro wa kuchinja wanyama
na ndege umeibuka katika wilaya ya Momba mkoani Mbeya na kuzua mvutano kati ya
Waislamu na Wakristo katika Mji wa Tunduma ambao ulizua maandamano ya wananchi
baada ya kubainika kuwa ng’ombe kadhaa walichinjwa na Mkristo na kusambazwa
kwenye mabucha ya mji huo.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwan Athuman, alisema kilichojitokeza ni kwamba kati ya
ng’ombe 38 waliochinjwa katika mji huo tisa ilielezwa kuwa zilichinjwa na
Mkristo.
Kamanda
Athuman alisema baada ya taarifa hizo kuenea mjini humo, watu ambao wana imani
tofauti walilalamikia suala hilo kwa viongozi na hivyo Kamati ya Ulinzi na
Usalama chini ya Mkuu wa Wilaya ya Momba, Abiud Saideya iliingilia kati kwa
kuzungumza na wachinjaji na wenye mabucha.
“Kimsingi
hakuna vurugu zozote zilizotokea Tunduma ni mvutano tu uliojitokeza wa kuchinja,
unajua kuna watu wanaombea vurugu zitokee Tunduma, tunashukru Kamati ya Ulinzi
na Usalama imelipatia ufumbuzi suala hilo ambalo pia lilijitokea na wilaya ya
Mbozi,” alisema.
Alisema Jeshi
la Polisi halikuchukua zozote za kupiga mabomu kwa watu walioamua kuandamana
kutokana jana kuwa sikukuu ya Pasaka.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Momba, Saideya, alisema kilichojitokeza ni kwamba siku ya Ijuma baadhi
ya Wakristo walipeleka maombi kwa Mkurugenzi wa Mji wa Tunduma wakitaka suala la
kuchinja wanyama lifanywe na wao badala ya kutumia
Waislamu.
Alisema ofisi
ya Mkurugenzi wa Mji wa Tunduma baada ya kupata taarifa hizo iliwajibu kuwa ombi
hilo wamelipokea watalifanyia kazi kwa kuwasiliana na viongozi wao wa juu kwani
tatizo hilo limekuwa la kitaifa hivyo wakaelekeza utaratibu wa zamani wa
kuchinja uendelee kama kawaida wakati wakisubiri utaratibu
mpya.
Saideya
alisema licha ya kupewa majibu hayo, baadhi ya Wakristo walikwenda kuchinja
ng’ombe wenyewe katika machinjio yaliyopo mjini Tunduma bila kusubiri maelekezo
mapya ya serikali kuhusu jambo hilo hali iliyozua malalamiko kutoka kwa watu
wengine.
Chanzo: Nipashe
Post a Comment