Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin
Mkapa
---
Dar. Ujumbe wa amani na tahadhari ya umakini kwenye
utoaji maoni kwenye Katiba ndiyo vilitawala wakati wa misa za Sikukuu ya Pasaka
zilizofanyika sehemu mbalimbali nchini jana na juzi.
Miongoni mwa waliotoa hotuba wakati wa sikukuu hiyo ni
pamoja na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ambaye alikuwa mkoani
Mtwara; na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyekuwa jijini Dar es
Salaam.
Mkapa akataa udini
Rais mstaafu Mkapa alitumia fursa ya kutoa salamu
katika Kanisa Katoliki mjini Masasi kuliasa taifa kujiepusha na utoaji wa maoni
ya Katiba kwa misingi ya dini.
Mkapa alisema katiba ijayo haipaswi kuwa na itikadi za
kidini kwa kuwa zinaweza kuliangamiza taifa.
“Wapo watakaopata uwakilishi kupitia rasimu ya Katiba
ya nchi. Namwomba Mwenyezi Mungu awape mwanga, muhakikishe jambo moja tu ambalo
litakuwa msingi mkubwa wa amani na maendeleo na umoja wa taifa
letu.
Watupatie Katiba ambayo inatoa fursa kamilifu ya kila
mtu kuwa na imani yake.
“Katiba inayoheshimu imani ya kikatiba na imani zote
zinazofanywa na wananchi wa Kitanzania…Vilevile ihakikishe kwamba dola au nchi
yetu haina imani rasmi kama vile nchi yetu isivyo ya kabila moja, hivyo
haiwezekani kuwa na Katiba ambayo inatambua kwa dhana au maandalizi ya vipengele
mbalimbali kwamba kuna udini, haiwezekani.”Kwa Habari zaidi Bofya
na Endelea......>>>
Post a Comment