Mtuhumiwa wa
wizi, Christopher Sanga ‘Chinga’ (30), amefariki dunia katika chumba cha
upasuaji katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga baada ya
kufyatuliwa risasi na polisi.
Taarifa kutoka hospitalini zinasema mtuhumiwa huyo
alijeruhiwa na risasi iliyompiga kwenye
nyonga kisha kutokea katikati ya makalio na alifariki dunia juzi wakati
madaktari wakijitahidi kuokoa maisha yake.
Kwa mujibu wa mke wa marehemu,
Halima Mlongo (27), askari polisi watano walifika nyumbani kwake wakiwa
wamevaa kiraia, huku wawili kati yao wakiwa na bunduki kila mmoja.
Alidai kuwa walipofika nyumbani hapo
waliianza kuikagua nyumba hiyo, huku yeye akiwa dukani baadaye
walimwamuru amtafute mume wake, yeye aliingia chumbani na kumweleza
mumewe kuwa ana wageni wanamsubiri nje.
Aliongeza kuwa “Askari hao walipiga
teke mara mbili na mlango ukafunguka kisha marehemu akajihami kwa
kumkata na fyekeo mmoja wa askari hao na mwingine kuoana mwenzake
amejeruhiwa, alimfyatulia mume wangu risasi moja na akaanguka chini huku
akivuja damu nyingi.”
Jirani wa marehemu, James Nkondya
ambaye alishuhudia tukio hilo alisema kuwa askari hao hawakumwarifu hata
mwenyekiti wao wa kitongoji ambaye alifika hapo baada ya askari hao
kumpiga risasi Chinga kisha kuondoka zao.
Ndugu wa marehemu huyo walifika
mjini hapa kutoka Makete, walikataa kuuchukua mwili wa marehemu na
kuandamana hadi Kituo cha Polisi wakitaka kuelezwa sababu ya kifo, huku
wakitishia kuwa iwapo polisi wakiamua kumzika wenyewe watakiona.
Baba mdogo wa marehemu, Damian
Mbilinyi alisema walipofika Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa waliambiwa
waonane na Ofisa Upeleleizi wa Mkoa, Peter Ngusa na kushindwa
kuafikiana katika mazungumzo yao, lakini baada ya kubanana nao polisi
walitoa ubani wa Sh1,000,000 na lita 200 za dizeli kuusafirisha mwili wa
marehemu kwenda Makete kwa maziko.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa,
Jacob Mwaruanda a mtuhumiwa alipigwa risasi wakati akipambana na polisi
waliotaka kumkamata kwa wizi.
Mwaruanda alisema askari huyo na
wenzake walifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo mali za Sh2.5 milioni, za
Kampuni ya Sumry Enterprises ya mjini Sumbawanga anaodaiwa kutenda Machi
27.
SOURCE::MWANANCHI
Post a Comment