Watoto wa Kijiji cha matumaini cha Mjini Dodoma wakifurahia zawadi ya asali waliyopewa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (mwenye miwani katikati) wakati alipotembelea kijiji hicho Aprili 23,2013.Kulia kwake ni Mbunge wa Viti Maalum na Mkurugenzi wa Mfuko wa Catherine Foundation, Catherine Magige ambaye pia alitoa zawadi mbali mbali kwa watoto wa kijiji hicho.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Picha juu na chini ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (mwenye miwani katikati) na Mbungewa Viti Maalum na Mwenyekiti wa Mfuko wa Catherine Foundation, Catherine Magige wakizungumza na watoto wa kijiji cha Mtumaini cha Dodoma wakati walipotoa zawadi za vyakula na vitu mablimbali kwa kituo hicho, Aprili 23, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mmoja wa watoto wa kijiji cha Matumaini cha Dodoma akifurahia pipi ambayo ilikuwa ni miongoni mwa zawadi nyingi za vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mke wa Waziri mkuu, Mama Tunu Pinda na Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Catherine Foundation kwa watoto wa kijiji hicho, Aprili 23, 2013.
Post a Comment