Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mpendae,alipowasili katika Tawi la CCM Meya,kutoa kadi za Chama kwa wanachama wapya wa chama hicho,akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Wilaya ya Amani Mkoa wa Mjini Unguja leo.
Kikundi cha sarakasi cha Jimbo la Mpendae ,wakionesha umahiri wa sarakasi katika viwanja vya Tawi la CCM Meya Wilaya ya Amani,wakati wa Mkutano wa wa wananchi wa Jimbo hilo uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Wanachama wa CCM Tawi wa Jimbo la Mpendae,wakiwa katika Mkutano wa kuwakabidhi kadi Wanachama wapya wa CCM, pamoja na Jumuiya za chama hicho,katika viwanja vya tawi la CCM Meya,Mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akimkabidhi Kadi Mwanachama Mpya wa UWT Subira khamis,huko Tawi la CCM Meya akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja pamoja na kutembela miradi mbali mbali ya Chama leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Vijana wa Kikundi cha UB40 cha Mpendae,wakiongozwa na Mohamed Salum Mohamed,baada ya kutoa burudani yao wakati wa Mkutano. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu ZNZ
Post a Comment