Promota Kinda Nangolo wa Namibia akimwaga Rais wa IBF/Africa Onesmo Ngowi wakati akiondoka nchini humo kuelekea Botswana!
Rais
wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati,
Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili katika jiji la Gaborone, Botswana
kupromoti ubingwa wa IBF wa Kimataifa katika uzito wa Bantam.
Bondia
wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia mwenzake kutoka nchini
Namibia Immanuel “Prince” Naidjala walitoka sare wakati wakishindania
ubingwa huo katika pambano lililofanyika katika jiji la Windhoek,
Namibia tarehe 20 Mei mwaka huu.
Ujio
wa Rais Ngowi ulikuwa unangojewa na wadau wengi wa ngumi katika nchi
hii tangu aitembelee Botswana mwaka 2002 wakati wa mpambano kati ya
bondia wa Botswana Thuso Kubamang na Peter Malinga kutoka nchini Afrika
ya Kusini.
Rais
Ngowi atakutana na viongozi wa serikali ya Botswana pamoja na wadau
mbalimbali wa ngumi na safari yake itaanzia jiji kuu la Gaborone mpaka
jiji la pili kwa ukubwa la Francistown ambako wadau wengi wa ngumi
wanamsubiri kwa hamu.
Nchi
ya Botswana ni nchi yenye msingi mzuri sana wa ngumi za ridhaa lakini
tatizo kubwa limekuwa ni namna ya kuwaendelza wanapofikia kikomo kwenye
ridhaa. Kikao cha Ngowi na viongozi wa serikali wa Botswana kitaweka
msingi mzuri wa namna ya kuwaendeleza mabondia wa Botswana.
Botswana
ni nchi inayopakana na Namibia kwa hiyo mpambano
wa Sekotswe na Naidjalaunategemewa kuwa na wapenzi wengi wa ngumi kutoka
katika nchi hizi mbili.
Post a Comment