DAR ES
SALAAM, Tanzania
SHIRIKA la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), linatarajia kushirkiki maonesho ya siku tatu
ya Huduma za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (The Muhimbili Day Exhibitions
2013), ambayo yanafunguliwa rasmi kesho Jumatano na Waziri wa Afya, Dk Hussein
Mwinyi.
Maonesho
hayo yanayoratibiwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), yatafikia tamati
Ijumaa Aprili 19, yakiwa na nia ya kutoa nafasi ya kukuza huduma zake kwa wateja
wake, kwa kushirikisha taasisi na kampuni mbalimbali zenye udau katika sekta ya
afya nchini.
Akizungumza
na Habari Mseto, Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga, alisema walipokea
mwaliko wa ushiriki wa maonesho hayo kutoka MNH na kisha kuthibitisha, wakimiani
ni fursa pana itakayotangaza huduma za shirika hilo ambazo zina uhusiano wa
karibu na sekta ya afya.
Aliongeza
kuwa, wanachama na wasio wanachama wa NSSF watapata fursa adhimu ya kujionea
utoaji na uendeshaji wa huduma mbalimbali, zilizo na udau na Sekta ya Afya, kama
vile Mafao ya muda mrefu na Mafao ya muda mfupi.
Aliongeza
kwa kuyataja mafao ya muda mfupi kuwa ni pamoja kuumia kazini, ambapo kuna namna
mbili za kuumia akizitaja kuwa ni kuumia kwa taratibu kunakotokana na kazi
husika na kuumia kwa ghafla kama vile kukatika mkono na viungo vingine vya
mwili.
Mafao ya
Uzazi kwa akina mama, mafao ya rambirambi katika mazishi ya mwanachama, mafao ya
uzeeni, mafao ya ulemavu haasa ulemavu utakaomtoa mwanachama moja kwa moja
kazini, pamoja na ya mirathi, ambapo mke/mume na watoto ndiyo wanawajibika
kumrithi mwanachama.
Maonesho
hayo ya kila mwaka yanahusisha wadau wa afya wanaotoa huduma za matibabu na
upasuaji, wataalamu wa mionzi, wafamasia, wamiliki wa maabara, maduka ya dawa,
wasimamizi wa taarifa za kitabibu na huduma nyinginezo za kitiba.
‘Muhimbili
Day Exhibitions’ ni maonyesho yanayotoa fursa ya kipekee kwa washiriki kuonyesha
bidhaa na huduma zao, ambayo pia ni jukwaa kamili la kujenga mahusiabno ya
kibiashara kati ya watoa huduma na wateja wao, ikiwamo kupokea maoni kutoka kwa
watumiaji wa bidhaa zao.



Post a Comment