Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko za kifo cha Mkuu wa
zamani wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Makame Rashid kilichotokea
juzi (Aprili 14 mwaka huu) kutokana na maradhi jijini Dar es
Salaam.
Rais wa
TFF, Leodegar Tenga amesema msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu
kutokana na mchango aliotoa Meja Jenerali Makame Rashid ikiwemo kuwa mlezi wa
timu ya Ruvu Stars wakati huo akiwa Kamanda (CO) wa Kikosi cha Ruvu
JKT.
Pia aliwahi
kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mdhamini (Trustee) wa TFF
wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) na wakati akiwa Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya katika miaka ya themanini alikuwa sehemu ya mafanikio kwa timu
ya Tukuyu Stars ya Mbeya iliyotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1987 ikiwa
ndiyo kwanza imepanda kucheza Ligi Kuu wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la
Kwanza.
TFF inatoa
pole kwa familia ya marehemu Meja Jenerali Makame Rashid, Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), na
kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo
mzito.
Maziko
yanatarajiwa kufanyika leo (Aprili 16 mwaka huu) nyumbani kwao mkoani Mtwara.
Mungu aiweke roho ya marehemu Sembwana mahali pema peponi.
Amina
VPL KUTIMUA
VUMBI VIWANJA VITATU
Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 17 mwaka
huu) kwenye viwanja vitatu huku vinara wa ligi hiyo Yanga wakifukuzia ubingwa
huo jijini Tanga.
Yanga
inayoongoza ligi ikiwa na pointi 52 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika
mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Athuman Lazi kutoka Morogoro kwenye Uwanja wa
Mkwakwani. Waamuzi wasaidizi wa mechi hiyo ni Michael Mkongwa wa Iringa na
Godfrey Kihwili wa Arusha wakati Kamishna wa mechi hiyo ni Godbless Kimaro
kutoka Moshi.
Kagera
Sugar na Toto Africans zitaumana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika
mechi namba 164 itakayokuwa chini ya mwamuzi Martin Saanya wa
Morogoro.
Uwanja wa
Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro, na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji
4,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mtibwa Sugar yenye pointi 33 na Oljoro
JKT yenye pointi 28.
Israel
Nkongo kutoka Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Hamis
Chang’walu (Dar es Salaam) na John Kanyenye (Mbeya). Kamishna wa mechi hiyo ni
Ramadhan Mahano kutoka Iringa.
AS FAR
KUWASILI KESHO KUIKABILI AZAM
Wapinzani
wa Azam katika michuano ya Kombe la Shirikisho, AS FAR Rabat ya Morocco
wanatarajiwa kutua nchini kesho (Aprili 17 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya
Emirates.
Msafara wa
timu hiyo wenye watu 28 utafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo,
Dar es Salaam tayari kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayochezwa
Jumamosi (Aprili 20 mwaka huu) saa 10 kamili jioni Uwanja wa
Taifa.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)



Post a Comment