Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013
akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli
ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe
Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013
akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli
ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe
Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013
akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William
Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika
mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko
ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013
akipozi na familia ya Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli
ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe
Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.Picha na IKULU
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto ambaye
alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Akiongea na mgeni huyo katika hoteli ya Seronera
iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara, Rais Kikwete
amempongeza Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi
wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Mhe Rais pia alimueleza Mhe Rutto furaha yake pamoja na
kuridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi
hiyo.
Alielelezea matumaini yake ya kuwa urafiki uliopo
kati ya Tanzania na Kenya utadumishwa pamoja na kusukuma mbele gurudumu
la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe Rutto, ambaye aliwasili mkoani Mara wiki
iliyopita akiwa na mke wake na watoto, ameondoka leo baada ya chakula cha
mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.
Mwisho
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
1
Aprili,
2013
Post a Comment