Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ametoa mipira
zaidi ya 1,200 yenye thamani ya dola 30,000 za Marekani kwa vyama vya mpira wa
miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na vituo 21 vilivyo hai vya kuendeleza vijana
(academies).
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) lilimpa Rais Tenga fedha hizo ikiwa ni
shukrani kwake kwa kushughulikia mgogoro wa uongozi wa mpira wa miguu nchini
Kenya uliodumu kwa miaka miwili; ambapo nchi hiyo kutokana na mgogoro huo
ilikuwa na vyama viwili (KFF na FKL).
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi mipira hiyo kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam leo
(Aprili 22 mwaka huu), Rais Tenga amesema amefanya hivyo kwa vile anaamini kuwa
mipira ndiyo kitu muhimu katika kuinua mchezo huo mahali
popote.
“Dhamira
yangi si kushukuru kwa hafla hii, bali kutoa sababu kwa nini nimefanya hivi.
Ninaamini kwa kuanzia mipira ndiyo muhimu, pili kwa kufanya hivi itaonekana
kweli mipira imegawiwa,” amesema Rais Tenga.
Amesema
amesema mpira wa miguu kwa Tanzania unahitaji sana watu wa kujitolea, na yeye
amefanya hivyo kwa kujitolea kutokana na ukweli shughuli anazotumwa na FIFA ni
za kujitolea.
Rais Tenga
ambaye pia alitumwa na FIFA kutatua matatizo ya uongozi wa mpira wa miguu katika
nchi za Uganda, Zambia na Sudan Kusini amesema anaamini anapata fursa hizo
kutokana na kuwa kiongozi wa TFF, na kwa kuwakumbuka waliomchagua ndiyo maana
hakusita kupeleka fedha hizo kwenye mipira.
Amesema
moja ya ndoto zake wakati anaingia kuongoza TFF mwaka 2004 ameshindwa kutimiza
ni kusaidia mipira, kwani uwezo wa kununua mipira kwa wanaocheza katika ngazi ya
chini hasa watoto haupo.
“Hizi
kelele zote za maendeleo ya mpira wa miguu ni kwa sababu shuleni hakuna vifaa.
Nia yangu ilikuwa shule zote zipate mipira, lakini hiyo ni moja ya ndoto
nilizoshindwa kutekeleza. Vipaji haziwezi kupatikana kama watoto
hawachezi.
“Tunashukuru
sana kwa Serikali kurejesha mpira shuleni. Hata nitakapoondoka madarakani
nikipata nafasi nitaendelea kuomba mipira kwa ajili ya shule,” amesema Rais
Tenga.
Vyama vya
mikoa ambavyo jumla ni 32 (Tanzania Bara na Zanzibar) kila kimoja kimekabidhiwa
mipira 25 (kumi saizi namba tano, 15 saizi namba nne kwa ajili ya vijana). Kwa
academies ambazo ni 21 kila moja imepewa mipira 25 (minane saizi namba tano, na
15 saizi namba nne).
Viongozi
waliohudhuria hafla hiyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) Almasi Kasongo, Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Mwanza (MZFA) Nassib Mabrouk na Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani
(COREFA) Riziki Majala.
Kwa upande
wa shule alikuwa Kanali mstaafu Idd Kipingu ambaye ni mmiliki wa shule ya Lord
Baden ya Bagamoyo mkoani Pwani.
COASTAL,
AZAM KUCHEZA SIKU YA MUUNGANO
Timu za
Coastal Union ya Tanga na Azam zitapambana Aprili 26 mwaka huu katika mechi ya
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) itakayofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga.
Awali mechi
hiyo namba 168 ilikuwa ichezwe Aprili 27 mwaka huu, lakini imerudishwa nyuma kwa
siku moja ili kuipa fursa Azam kujiandaa kwa mechi ya marudiano ya raundi ya
pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya
Morocco.
Mechi hiyo
itachezeshwa na Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani akisaidiwa na Abdallah Mkomwa
(Pwani), Vicent Mlabu (Morogoro) wakati mwamuzi wa mezani atakuwa Mohamed Mkono
wa Tanga. Charles Komba wa Dodoma ndiye atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo ya
raundi ya 24.
Baada ya
mechi ya Tanga, Azam itarejea Dar es Salaam siku inayofuata tayari kwa safari ya
kwenda Rabat itakayofanyika Aprili 28 mwaka huu. Mechi hiyo itachezwa wikiendi
ya Mei 3, 4 au 5 mwaka huu.
Keshokutwa
(Aprili 24 mwaka huu) kutakuwa na mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya African
Lyon na JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es
Salaam.
Iwapo Azam
itafanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kutakuwa na
marekebisho ya ratiba ya VPL. Hiyo ni kutokana na raundi inayofuata ya Kombe la
Shrikisho kuchezwa wikiendi ya Mei 17, 18 na 19 mwaka huu ambapo bado
haijajulikana Azam itaanzia wapi (nyumbani au ugenini) iwapo
itavuka.
Mechi
nyingine za VPL mwezi ni Aprili 25 (Ruvu Shooting vs Simba- Uwanja wa Taifa), na
Aprili 28 (Simba vs Polisi Morogoro- Uwanja wa Taifa).
MKUTANO WA
WAANDISHI WA HABARI
Kocha Mkuu
wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Kim Poulsen atakuwa
na mkutano na waandishi wa habari kesho (Aprili 23 mwaka
huu).
Mkutano huo
utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF).
WAMOROCCO
WA AZAM WAINGIZA MIL 50/-
Mechi ya
kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na AS FAR Rabat ya
Morocco iliyochezwa juzi (Aprili 20 mwaka huu) imeingiza sh.
50,850,000.
Fedha hizo
katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa
timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 8,268 waliokata
tiketi.
Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000
ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A. Kiingilio cha sh. 5,000
ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 7,354.
Mgawo
ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja
sh. 6,791,175, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 4,527,450 na asilimia 75
iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 33,955,875.
Mechi
iliyopita ya Azam katika michuano hiyo dhidi ya Barrack Young
Controllers II ya Liberia iliingiza sh. 44,229,000 kutokana na watazamaji 17,128
waliokata tiketi. Viingilio vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh.
20,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP
A.
MECHI YA
JKT RUVU, YANGA YAINGIZA MIL 66/-
Mechi ya
Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Yanga iliyochezwa jana (Aprili 21 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,568,000 kutokana na
watazamaji 11,864.
Viingilio
katika mechi hiyo namba 106 iliyomalizika kwa Yanga kutoa dozi ya 3-0 kwa
wenyeji wao vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila
klabu ikipata mgawo wa sh. 15,702,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 10,154,440.68.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,984,450.40, tiketi sh.
3,183,890, gharama za mechi sh. 4,790,670.24, Kamati ya Ligi sh. 4,790,670.24,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,395,335.12, Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 931,519.21 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA) sh. 931,519.21.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment