Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mfuko huo kutimiza miaka 10 tangu
kuanzishwa kwa Fao la Elimu. Kulia ni Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele na
Meneja Michango wa PPF, Cosmas Sasi. (Picha na Habari Mseto Blog)
Baadhi ya
wafanyakazi wa PPF.
DAR ES
SALAAM, Tanzania
MFUKO wa
Pensheni wa PPF, umetambia mafanikio iliyopata katika kipindi cha miaka 10 ya
Fao la Elimu, linalotolewa kwa kuwasomesha watoto, huku likijumuisha ulipaji wa
karo za shule na mahitaji mengine ya wanafunzi.
Akizungmza
na Habari Mseto, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, alisema kuwa Fao la Elimu
la PPF lilianza kuwasomesha wanafunzi mwaka 2003, ambapo mwaka jana 2012 pekee
jumla ya wanafunzi 1,333 walisomeshwa katika shule tofauti za
sekondari.
Erio
alibainisha kuwa, PPF ilitumia kiasi cha shilingi milioni 682, kuwalipia karo na
mahitaji mengine wanafunzi inaowasomesha waliopo katika shule 765 za sekondari
kote Tanzania Bara na Visiwani na kufaulisha wengi miongoni
mwao.
Aliongeza
kuwa, sherehe za mafanikio yatokanayo na Fao la Elimu zimeanza katika kanda zote
nchini na kwamba zitahitimishwa Jumamosi Aprili 27 katika sherehe za kitaifa,
ambazo mgeni rasmi atakuwa ni mke wa Rais, Mama Salma
Kikwete.
Pamoja na
sherehe hiyo itakayoambatana na burudani za aina mbalimbali, PPF itatoa zawadi
kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani iliyopita, miongoni mwa wale
wanaosomeshwa kupitia Fao la Elimu la mfuko wake.
“Lengo la
zawadi hizo kwa wanafunzi hao ni kuwahamisha wengine watumie vema fursa ya
kusomeshwa kupitia Fao la Elimu ili wafanye vizuri katika mitihani yao ijayo na
tunawaomba wote wanaosomeshwa na PPF waje kwenye sherehe hiyo,” alisisitiza
Erio.
Aidha, Erio
alifichua kwamba, licha ya matokeo mabaya ya mitihani ya mwaka jana yaliyotokana
na ugumu wa mitihani hiyo, watoto waliokuwa wanasomeshwa na PPF waliweza kufanya
vizuri, kiasi cha kuwapo waliofaulu kwa daraja la kwanza na
pili.
Post a Comment