Saluti
Jembe Letu: Wachezaji wa
Manchester United wakimpongeza mshambuliaji wao Robin van Persie (kushoto) baada
ya kufunga moja ya mabao yake matatu, yaliyoipa United ushindi wa 3-0 dhidi ya
Aston Villa na kutawazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya England, taji lililokuwa
likishikiliwa na mahasimu wao Man City.
Kiduku cha
Ushindi na Utamu Wake: Mholanzi, Robin van Persie (katikati),
akishangilia kwa staili ya kucheza muziki baada ya kuiwezesha timu yake kushinda
dhidi ya Aston Villa na kutwaa jtaji la 20 katika historia ya Man United, ambalo
ni la 13 chini ya Mskochi Sir Alex Ferguson.
Ubingwa wa
Uzeeni Mtamu Bana: Beki mkonngwe Rio Ferdinand (kulia), akiongoza
ushangiliaji na wachezaji wenzake wakiwa wamejifunika bendera ya Man
United
Duuh, Hawa
Watoto Noma Aisee: Alex Ferguson (wa pili kulia) akishangilia na jopo
lake la Maofisa wa Benchi la Ufundi na wachezaji wa akiba, mara baada ya filimbi
ya mwisho ya mechi dhidi ya Aston Villa.
Furaha ya
Nahodha Mfaransa: Beki wa kimataifa wa Ufaransa anayeiongoza Man United
kwa sasa, Patrice Evra, akishangilia huku akiwa amejifunga bendera ya timu yake
kichani.
Pozi la
Picha na Shujaa wa Msimu: Ferdinand, akiwa na nyota wengine wakipozi kwa
picha na Robin van Persie aliyeibuka shujaa wa msimu wa klabu hiyo, ambapo jana
alifunga mabao yote matatu 'hat-trick.'
Utu Uzima
Dawa: Yoso Mbrazil wa Man United, Rafel da Silva (kushoto) akipiga picha
na beki mkongwe wa klabu hiyo, Rio Ferdinand.
Bao la
Kwanza Nalifunga kama Ifuatavyo: Van Persie (kushoto) akipiga shuti
kufunga bao la kwanza katika mechi hiyo iliyowapa ubingwa wa Ligi
Kuu.
Fundi
Kazini: Van Persie akipokea na kupiga kufunga bao la pili la Man United
dhidi ya Aston Villa.
Huwezi
Kuzuia Mvua Weweee!! Van Persie hapa anaonekana akimaliza kazi kwa
kufunga bao la tatu la United.
Sisi Ndio
Sisi, Wengine Mafisi: Wachezaji wa Man United wakishangilia ubingwa wa
Ligi Kuu.
Jezi ya
Mtaalam Wenu Hii Hapa: Van Persie akionesha jezi yake, ambayo pia
inawakilisha idadi ya vikombe vya Ligi Kuu vilivyobebwa na Man
United.
Shampeni
ya Ushindi Hiyoooo!! Rio Ferdinand akitingisha na kuwamwagia wenzake
shampeni ya kusherehekea ubingwa wa Ligi Kuu.
Nina
Furaha Kuliko Nyie Wote: Ferdinand akiruka juu kwa furaha wakati wa
zoezi la kufungua shampeni ya kushangilia ubingwa.
Hii Yangu
Pekee: Ferguson akifungua shampeni yake ya kusherehekea ubingwa na kisha
kuanza kuinywa kama anavyoonekana katika picha ya chini.
Post a Comment