Habari kutoka Liwale, mkoani Lindi, zinasema kwamba hali si shwari
wilayani humo usiku huu kufuatia fujo kubwa zinazofanywa na wanaodaiwa kuwa
wakulima wa korosho wanaodai malipo yao.
Nyumba nne inasemekana zimeshachomwa moto na ng'ombe kadhaa
wamechinjwa na watu hao. Polisi wameshawasili eneo hilo na mabomu ya kutoa
machozi yameanza kurindima katika harakati za kutawanya watu hao.
Habari hizo zinasema nyumba mbili za Mbunge wa Liwale na Mbili za mwenyekiti na makamu wa Umoja AMCOS zimechomwa moto, wakati ng'ombe wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya na za meneja wa Ilulu Union wamechinjwa.

Credits: MichuziBlog
Post a Comment