MWILI
WA ALIYETUHUMIWA KWA MAUAJI YA MTOTO AYUBU AGEN UKIWA UMECHOMWA MOTO NAWANANCHI
WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUMKUTA MITA CHACHE KUTOKA KWENYE MWILI WA MAREHEMU
AKIWA NA KISU KINACHODHANIWA KUTUMIKA KATIKA
MAUAJI
|
MWILI WA MTOTO AYUBU UKITOLEWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANAWILAYA YA RUNGWE |
SAFARI
YA KUELEKEA KIJIJI CHA IJOKA KWA MAZISHI
-wananchi
wapanda hasira wamteketeza kwa moto mtuhumiwa.
MATUKIO ya kutisha na
ya kinyama dhidi ya watoto wadogo yameendelea kuutikisa Mkoa wa Mbeya, baada ya
mwanafunzi wa chekechea, Ayoub Agen (6) kuuwa kwa kuchinjwa mithili ya kuku na
wauaji kuondoka na kichwa chake.
Hata hivyo wananchi
wenye hasira walifanikiwa kumnasa mmoja wa watuhumiwa wa tukio hilo, ambaye hata
hivyo jina lake halikuweza kupatikana ambapo baada ya kummbana ili aeleze sehemu
walikokificha kichwa cha marehemu aligoma hivyo kuamua kumteketeza kwa
moto.
Habari za uhakika
kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Ijoka katika
kata ya Mpombo, wilayani Rungwe, Rafael Mwaikenda, zinadai kuwa tukio hilo
lilitokea Machi 31 majira ya saa 11:00 jioni.
Akifafanua zaidi
Mwenyekiti huyo alisema, marehemu Agen alikuwa ni mwanafunzi wa chekechea
katika shule ya msingi Lusanje kijijini hapo na kwamba alikutwa na mauti hayo ya
kikatili baada ya watu hao wasiofahamika kufanikiwa kumuiba nyumbani
kwao.
Mwaikenda alisema
mwili wa marehemu uliokotwa ukiwa umetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku
kichwa kikiwa hakionekani hadi sasa ikiwa ni muda mfupi tu baada ya watu hao
wasiofahamika kumwiba toka nyumbani kwa wazazi wa marehemu
.
“Marehemu alichukuliwa
na watu hao wasiofahamika akiwa anacheza na wenzake na wenzake baada ya kuona
hivyo waliamua kutoa taarifa ambapo muda mfupi walianza kumtafuta bila
mafanikio, lakini wananchi wakiwa wanaendelea na harakati hizo waliukuta mwili
huo ukiwa umetelekezwa kichakana na wauaji hao kuondoka na kichwa” alifafanua
Mwaikenda.
Mkazi mwingine katika
kijiji hicho, Tumpale Sankemwa, alikielezea mkasa huo, alisema baada ya wananchi
kugundua mwili huo wa marehemu waliendelea kuwasaka wahusika na wakiwa katika
harakati hizo ghafla walikutana na mtu mmoja ambaye walimtilia
mashaka.
Alisema baada ya
kumfanyia mahojiano ya kina kwa kuwa alikuwa hafahamiki na mgeni kijijini hapo,
alikuwa akijibu jeuri hivyo kuwapandisha hasira wananchi jambo lililosababisha
kuanza kumshambulia na hatimaye kumuua papo
hapo.
Hata hivyo alisema
wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigon mtu huyo licha ya kutotaja jina
lake, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa kueleza kuwa waliohusika walikuwa
watatu na kwamba wenzake walikuwa wameondoka.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi,Diwani Athumani, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa kichwa cha marehemu huyo
hakijaonekana na jeshi hilo linaendelea kufanya
uchunguzi.
“Ni kweli tukio hilo
limetokea, hata hivyo mtu anayetuhumiwa kushiriki mauaji hayo naye aliuawa kwa
kupigwa na wananchi wenye hasira ambao licha ya kumuua waliuteketeza mwili wake
kwa moto”.
Aliongeza kuwa
mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mwanaume anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 30 hadi
35 na kwamba uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha mauaji hayo kinahusishwa
na imani za kishirikina.
Wakati huo huo watu
watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya, katika matukio
mawili tofauti ya ajili za barabarani mkoani
hapa.
Katika tukio la kwanza
lililotokea eneo la Mbalizi wilayani hapa, majira ya saa nne usiku katika
barabara ya Mbeya- Tunduma, watu wawili, Meshaki Inkuru (24) na Said Ndasi (19)
baada ya gari aina ya Toyota Chesser yenye nambari za usajili T 516 AAA
lililokuwa likiendeshwa na mtu asiyefahamika kuwavamia wakiwa nje ya Hoteli ya
Royal Tughimbe walikokuwa wakiendelea na sherehe za
Pasaka.
Kamanda wa polisi
aliwataja majeruhi wa tukio hilo ambao wamelazwa katika Hospitali teuli ya
wilaya ya Mbeya ya Ifisi ni Shar Mkumbwa (20), Juliet Katemi (18) wote wakazi
wa mji mdogo wa Mbalizi.
Tukio lingine ni lile
lililotokea eneo la Soweto ambapo mtu mmoja mtembea kwa miguu, aliyetambuliwa
kwa jina moja la Paul (60) kufa papo hapo baada ya kugongwa na gari ambayo hata
hivyo haikuweza kufahamika mara moja .
SOURCE MBEYA
YETU
|
1 comments:
Mbeya kunatisha kweli Jamani Watanzania Unyama huu hadi lini hasa? Poleni sana wanafamilia kwa Misiba hiyo
ReplyPost a Comment