Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SHEREHE SIKU YA WATOTO YATIMA, WAGONJWA ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohd Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine wa serikali na dini ya Kiislam, wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima walioiwakilisha Zanzibar mwaka jana katika Tamasha maalum la watoto yatima. Picha hiyo imepigwa kwenye sherehe za watoto yatima zilizofanyika hoteli ya Bwawani.
Viongozi wa Kitaifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Muzdalifah Zanzibar, katika hafla ya sherehe za watoto yatima zilizofanyika hoteli ya Bwawani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokea zawadi kutoka kwa muwakilishi wa shirika la IHH la Uturuki katika hafla ya sherehe za watoto yatima zilizofanyika hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimjuilia hali Sheikh Habib Ali Kombo nyumbani kwake Kiembesamaki. Hii ilikuwa ziara maalum ya kuwatembelea wafiwa na wagonjwa katika manispaa ya Zanzibar,
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Muzdalifah Zanzibar, katika hafla ya sherehe za watoto yatima zilizofanyika hoteli ya Bwawani Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar Sheikh Abdallah Hadhar.
Viongozi wa Kitaifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya IHH ya Uturuki na Jumuiya ya Muzdalifah Zanzibar, katika hafla ya sherehe za watoto yatima zilizofanyika hoteli ya Bwawani, tarehe 30/03/2013.
(picha na OMKR).

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top