Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SIMBA YASINDIKIZA UBINGWA WA YANGA BAADA YA KUDROO 2-2 NA AZAM FC


Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Azam Fc, David Mwantika, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2.
Haruna Chanongo (katikati) akianguka baada ya kuwaramba chenga mabeki wa Azam Fc na kukwatuliwa karibu kabisa na eneo la hatari.

Haruna Chanongo, akijiandaa kupiga shuti.
Mwinyi Kazimoto (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa Azam Fc, wakati wa mchezo huo.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba (kulia) akimtoka beki wa Azam Fc, Himid Mao, wakati wa mchezo huo.
Kocha Msaidizi wa Simba, Julio (kulia) akimlalamikia Kamisaa wa mchezo huo, baada ya kuona mwamuzi wa mchezo huo, Oden Mbaga, akichezesha ndivyo sivyo.
Mafadha wa Simba wakiwa kwenye Benchi huku vijana wakiwajibika uwanjani wakati wa mechi hiyo.
***********************************************
MABAO mawili ya Simba katika mchezo wao dhidi ya Azam FC uliomalizika
kwa sare ya mabao 2-2 imeipalilia ubingwa kwa Yanga kwa kuisimamisha
Azam ambao walikuwa wanatishia ubingwa huo.

Matokeo hayo ni faida kwa Yanga ambayo kwa sasa inahitaji pointi sita
(kwa kutegemea matokeo ya Azam FC) ili itangaze ubingwa kwani ikishinda
michezo hiyo itafikisha pointi 58 ambazo haitafikiwa timu yoyote katika
ligi hiyo.

Azam sasa wamebaki katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 47 huku Simba
wakiwa wamefikisha pointi 36.

Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika
dakika ya 12 mfungaji akiwa Ramadhani Singano aliyemalizia kazi nzuri
iliyofanywa na Mrisho Ngassa baada ya kuwatoka walinzi wawili wa Azam
FC, Joakins Atudo na Lackson Kakolaki kabla ya kumtengenezea nafasi
nzuri ya kufunga Ramadhan "Messi" Singano na kumchambua kipa wa wauza
Ice Cream, Mwadini Ali Mwadini.

Bao hilo liliwachanganya wachezaji wa Azam FC na kuwapa mwanya 'watoto'
wa Simba SC kutawala mchezo na kupachika bao la pili ya sita baadaye
kufuatia ushirikiano kati yake na Haruna Chanongo na Ngassa tena kumtoka Kakolaki na kabla ya kumpa pasi safi Singano na kufunga kirahisi.

Kuona jahazi linakwenda mrama, kocha wa Azam FC ambaye awali alichezesha mabeki watano nyuma, alimtoa Kakolaki na nafasi yake kuchukuliwa na Khamis Mcha ambaye alibadili mchezo na kupata bao la
kwanza dakika ya 29 kwa njia ya penati iliyofungwa kifundi na Kipre
Tchetche.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kushambulia zaidi na huku 'watoto' wa Simba SC wakionekana kushindwa kuhimili vishindo na kuruhusa bao la kusawazisha katika dakika 71 kupitia kwa Humphrey Mieno kwa njia ya 'mkono' akimalizia mpira wa faulo wa Mcha.

Wachezaji wa Simba SC walimzonga mwamuzi Oden Mbaga wakilalamikia bao
hilo na mwamuzi huyo ambaye alionekana 'kupendelea' wapinzani wa Simba
 
credits: Sufiani Mafoto
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top