Ndugu waandishi wa
habari;
LEO tumewaita hapa ili
kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba nikiwa mwanasheria na mtu
ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu, nimefanya uchunguzi matukio haya ya
utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi mno.
Uchunguzi huu nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa
kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na Usalama, Willifred Muganyizi Lwakatare, ambaye
hivi sasa anashitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.
Nimefanya hivyo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa
langu na chama changu. Katika uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi
ikiwamo kuwapo kwa genge la watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM),
wanaopanga mipango hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu
wengine.
Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi na Mwigulu
Nchemba, “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi la polisi Desemba
mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote wala kumhoji, hadi pale
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, alipovamiwa na
kuumizwa.
Aidha, Nchemba amedai kumiliki video ile Desemba mwaka
jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii (YouTube na Jamii
Forum) baada ya kutekwa kwa Kibanda. Hapa mtu makini anaweza kujiuliza, hiki
kimelenga nini?
Kwamba genge hili la kina Nchemba na wenzake,
walipanga kumteka Kibanda, wakatimiza lengo lao hilo, baadaye wakaingia kwenye
plani B ya kutaka kuihusisha Chadema. Wakamtumia Ludovick Joseph Rwezahula
ambaye ni mshitakiwa wa pili katika kesi ya Lwakatare, kufanikisha mkakati wao
huu wa kishetani.
Ndugu waandishi wa habari;
Huu ni mchezo mchafu na
wahatari mno ambao kwa vyovyote vile, haupaswi kuvumiliwa. Kuanzia sasa nimeamua
kwa dhati kabisa, kukomesha mchezo huu ambao unahatarisha uhai wa taifa
letu.
Kwa kuanzia, kesho Jumatatu, nitaongoza jopo la
mawakili sita wa Chadema kumtetea Bw. Lwakatare. Wenzangu wengine katika kesi
hii, ni Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu, Edson Mbogoro, Peter Kibatara na
Nyaronyo Kicheere. Huko mbele tutaongeza mawakili wengine, akiwamo mmoja
anayewekwa na familia ya Lwakatare.
Ndugu waandishi wa habari;
Mnaweza kujiuliza, kwa nini Chadema kimechukua uamuzi
huu wa kuweka kundi kubwa la wanasheria katika kesi hii ya Lwakatare? Jibu ni
kwamba tumegundua kuwa kesi hii imefunguliwa kwa lengo maalum la kuidhoofisha
Chadema na kuinusuru CCM ambayo inakabiliwa na dhahama ya kushindwa katika
uchaguzi mkuu ujao kutokana na kushamiri kwa makundi.
Hivyo wameamfungulia kesi Lwakatare, kwa lengo la
kutaka kuaminisha umma kuwa Chadema ni chama cha magaidi, kinapanga ugaidi na
hivyo kichukiwe. Hilo ndilo lengo lao. Basi!
Ndugu waandishi wa habari;
Pili, nitakwenda mahakamani kuwasilisha ombi maalum la
kuomba amri ya mahakama kuagiza makampuni ya simu za mkononi kuwasilisha
mahakamani statement za simu za watu kumi (10) ili kusaidia mahakama kutenda
haki na jamii kujua ukweli wa mambo haya.
Watu ambao nitaomba mahakama itoe amri ya kuletwa
taarifa zao simu
na meseji (sms) ni Naibu
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka, anayetumia simu Na.
255756809535, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Lameck
Nchemba, anayetumia simu tano zikiwamo 0754 008888, 0757 946223, 0714 008888 na
0787 513446 na Ludovick Joseph Rwezahula, ambaye simu zake ni,0715 927100 na
0753 927 100.
Mwingine ambaye mawasiliano yake yanahitajika, ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi, anayetumia simu Na. 0754
003388, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Mwananchi, Dennis Msaky anayetumia simu
mbili, 0655 331010 na 0764 331010 na Bw. Sinbad Mwagha, ambaye ni afisa wa idara
ya usalama wa taifa, anayetumia simu 0754 006355.
Wengine, ni Bw.
Shaali Ali, afisa mwinge wa usalama wa taifa anayetumia simu Na. 0716990099,
Saumu K. Malungu, mwenye kutumia simu 0719 541 434 na 0789 614 629, simu mbili
zinazotumiwa na mtuhumiwa mkuu wa utekaji wa Dk. Steven Ulimboka, Bw. Ramadhani
Abeid Igondo ikiwamo 0713 760 473, simu za Bw. Ridhiwani Kikwete ambazo ni 0754
566299, 0784 566 299, simu ya Dr. Steven Ulimboka, ambayo ni 0713 0713 731 610,
pamoja na simu zote tatu za Willifred Lwakatare, ambazo ni 0786 774697, 0713
237869 na 0758 417169.
Ndugu waandishi wa habari;
Mtu mwingine muhimu nitakayeomba mahakama itoe amri ya
kutolewa kwa taarifa zake, ni mwandishi wa habari na mpigapicha wa magazeti ya
serikali, Muhidini Issa Michuzi. Mwandani huyu wa Ikulu, ndiye aliyeandika
ujumbe kwa njia ya emeili kuipongeza ofisi binafsi ya rais (OBR) na usalama wa
taifa kwa kupata video ya Lwakatare.
Pongezi za Michuzi kwa TISS ndizo zinanisukuma kuiomba
mahakama kuagiza kupatikana taarifa zake. Michuzi anaipongeza TISS kwa kuibua
njama za wahalifu, lakini mimi ninajua TISS ikipata njama za aina hiyo haraka
inapeleka ushahidi polisi, lakini huu wa Lwakatare ulipelekwa Youtube, badala ya
kwenye vyombo vya sheria.
Maneno ya Michuzi kwamba ni TISS imeibua hiyo video
yanathibitisha ushiriki wa TISS kwenye mchezo huo mchafu, na kwamba Chadema
kinajua kuwa Michuzi alishirikiana na watu wa usalama wa taifa katika kazi hiyo
chafu. Software za video (editing) walizotumia zilitoka kwake. Fedha ya kuandaa
hiyo video zilitoka usalama na Ikulu. Tunajua kuwa wale vijana wa Ada Estate na
yule jamaa anayempelekea kigogo wa Jamii Forum, walilalamika sana kwa mmoja wa
wamiliki wa JF.
Ndugu waandishi wa habari;
Chadema kinajua kuwa
mmoja wa watuhumiwa hawa, Mwigulu Nchemba anafanya mipango na baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom ili kumsaidia kufuta taarifa zake. Nachukua
nafasi hii, kuionya kampuni hiyo kuacha kucheza mchezo huo kwa kuwa ni kinyume
cha sheria za mamlaka ya mawasiliano (TCRA).
Tunahitaji mawasiliano haya kwa kuwa Mwigulu –
zinaonyesha mtuhumiwa huyo akifanya mawasiliano mfululizo na Ludovick, yakiwamo
yale ya tarehe 4 Machi 2013. Hii ilikuwa siku moja kabla ya Kibanda
kutekwa.
Ndugu waandishi wa habari;
Hawa niliowataja ni watu
muhimu sana katika upangaji wa mkakati wa utengenezaji wa video ya Lwakatare na
vitendo vya kihalifu vya utekwaji wa Kibanda na tukio la kutekwa na kisha
kutupwa msutuni kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari nchini, Dr. Steven
Ulimboka.
Kwa mfano, simu ya Mwigullu Nchemba, namba 0714
008888, 0756 008888 na 0757 946223, zimefanya mawasiliano mara kadhaa na
Ludovick Joseph, Saumu K. Malungu, Jack Zoka, Ali Shaali na Ramadhani Ighondo.
Mawasiliano hayo yalifanyika katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari
ulishamiri; baadaye yakarudi tena kati ya 26 Desemba mwaka jana na 15 Machi
mwaka huu.
Miongoni mwa
mawasiliano ambayo tunaona yanahusika na ujambazi huu, ni yale ya 28 Desemba,
siku ambayo mkanda wa Lwakatare umerekodiwa; tarehe 4 hadi 6 Machi 2013, siku
moja kabla ya Kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane (saa 8:17) wa 13 Machi
2013, ambako mchana uliofuata Lwakatare alikamatwa.
Huyu Mwagha ndiye
aliyekuwa anatumika kuwasiliana na Saumu Malungu, ambaye tulimtaja kuwa ndiye
aliyekuwa amepewa kazi na Mwigulu na usalama wa taifa, kurubuni vijana wetu kwa
fedha ili kutoa ushahidi wa uongo juu ya video ya
Lwakatare.
Vilevile, mawasiliano ya Mwiguluna Mwagha, katika
kipindi hicho nayo tunayahitaji. Kwa sababu, huyu Mwagha anayetumia simu
0754006355, mbali na kuwasiliana na Mwigulu, ndiye aliyekuwa anawasiliana na
mmoja wa waliomteka Ulimboka; na ndiye aliyewasiliana na Saumu kati ya 20Januari
na Machi 6 mwaka huu.
Ndugu waandishi wa habari;
Ludovick alifanya
mawasiliano ya mwisho na Joyece Agustine, ambaye anatumia simu Na. 0717 559210,
mawasiliano ambayo yalifanyika saa 5:13 usiku. Hiyo ndiyo ilikuwa simu yake ya
mwisho usiku huo; katika siku hiyo Ludovick aliwasilisna na Joyce mara tisa
kuanzia saa 12: 54 asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mtandao wa Jamii
Forum, ambako video ya Lwakatare ilitumwa, Ludovick alikamatwa Machi 15 mwaka
huu. Hata hivyo, rekodi katika simu yake Na. 0715 927100 inaoyesha 17 Machi
Ludovick alifanya mawasiliano na Joyce Augustino. Mawasiliano hayo yalifanyika
saa 8: 9 usiku, wakati inadaiwa na polisi alishakamatwa.
Naye mhariri wa Mwananchi, Bw. Msaky ambaye anatajwa
kutaka kutekwa na Ludovick na Lwakatare, amekuwa na mawasiliano kadhaa na
Ludovick – mtu anayepanga kumteka. Ludovick na Msaky walifanya mawasiliano
mfululizo kati 27 Desema 2012, siku moja kabla ya video ya Lwakatare
haijarekodiwa na 7 Machi siku moja baada ya Kibanda kutekwa.
Msacky alitumia simu zake hizo mbili (0764 331010 na
0655 331010) kuwasiliana na Ludovick, huku Ludovick akitumia 0753927100.
Mawasiliano ya 31 Desemba yalifanyika Ludovick akiwa Tegeta, jijini Dar es
Salaam. Mawakala hawa wawili wa usalama wa taifa (Ludovick na Msaky), walikutana
31 Desemba 2012, katika hoteli ya Tamal, Mwenge jijini Dar es
Salaam.
Ndugu waandishi wa habari;
Baada ya kupitia taarifa
hizi za mawasiliano ya simu za Mwigulu Nchemba, Ludovick Joseph, Ramadhani
Ighondo na Saumu Malungu tumegundua yafuatayo: Kwamba, Ramadhani Ighondo,
amefanya mawasiliano mara nyingi na Mwigulu, Mwagha na Zoka; naye Mwagha
amefanya mawasiliano na Mwigulu na Saumu; naye Saumu amefanya mawasiliano na
Mwagha, Mwiguluna Shaali Ali, ambaye ni afisa usalama wa
taifa.
Tumegundua vilevile, kuwapo mawasiliano kadhaa kati ya
Ludovick na Msaky; Ludovick na Mwigulu; Msaky na Nchimbi; Msaki na Mwagha, Samu
na Mwagha na Ramadhani Ighondo Abeid, anayetuhumiwa kumteka Dk. Ulimboka na
Mwanga na Mwigullu.
Tumegundua pia kuwapo mawasiliano kati ya Ulimboka na
Ramadhani; Zoka na Ighondo na Ridhiwani na Ighondo. Mawasiliano haya yalifanywa
mfululizo usiku wa Juni 2012 siku ambayo Dk. Ulimboka alitekwa.
Tumepata kufahamu pia kwamba baadhi ya watu waliotajwa
na gazeti la MwanaHALISI kuwa waliwasiliana na Ighondo usiku wa Juni 26, mwaka
2012, wamefanya mawasiliano pia na Mwigulu, Mwagha na Shaali Ali.
Ndugu waandishi wa habari;
Mwagha ni afisa usalama
wa taifa anayefanyakazi makao makuu ya idara hiyo. Ndiye yule anayetumika
kuendesha michezo ya kuhonga wanasiasa wa CCM na upinzani. Ni Mwagha anayepanga
wabunge na kuwapanga waongee nini kwa maslahi ya CCM. Ushenzi wote anaoongea
Mwighulu bungeni, hupewa na Mwagha kwa maelekezo ya Jack
Zoka.
Naye Shaali ndiye aliyekutana na afisa wetu wa
usalama, Ahmed Sabula na mwenzake, Machi 29 mwaka huu katika hoteli ya See Cliff
jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo kati ya Sabula, kijana wetu wa usalama
na afisa usalama wa serikali Bw. Shaali alitaka Sabula akubali kutumika kwa
kutoa taarifa za vikao vya chama, kuwasilisha kwake nyaraka za kamati kuu na
kueleza mipango ya chama katika kesi ya Lwakatare.
Kwenye mpango huu, afisa huyo wa usalama wa taifa
ambaye ninamfahamu vizuri, alimuahidi Sabula kiasi cha Sh. milioni 30 na kwamba
fedha hizo angelipwa wiki iliyopita. Aliahidiwa pia kwamba kila nyaraka
atakayopeleka atalipwa ujira.
Aidha, Sabula aliahidiwa kulipwa shilingi 500,000
(laki tano) kila mwezi; afisa wetu huyu ameripoti tukio hilo kwa viongozi wake
wa chama. Yule mwenzake aliandaliwa kuwa shahidi wa kesi ya Lwakatare; aliambiwa
akikubali dili hiyo atalipwa kila mwezi Sh. 500, lakini akaombwa kuwa mvumilivu
kwa kuwa atalazimika kupotea kwa miezi kama mitano hadi sita.
Ndugu waandishi wa habari;
Kitendo cha Mwigulu kuwasiliana Ramadhani Ighondo,
Mwigulu kuwasiliana na Ludovick, Saumu kuwasiliana na Mwigulu, Ighondo
kuwasiliana na Ulimboka, Zoka kuwasiliana na Ighondo, tena katika muda uleule
ambao Ighondo amewasiliana na Ulimboka na Saumu kuwasiliana na Mwagha, ni
uthibitisho tosha kwamba usalama wa taifa wako nyuma ya mipango hii ya michafu
ya kupanga utekaji na kisha kutaka kukichafua Chadema.
Aidha, kitendo cha Ludovick kuwasiliana Msaky; Ighondo
kuwasiliana na Mwagha, Ridhiwani Kikwete kuwasiliana na Ighondo, tena kila baada
ya Ighondo kuwasiliana na Ulimboka na Jack Zoka, ni uthibitisho mwingine kuwa
genge hili la wahalifu linashirkiana na baadhi ya watu kutaka kuangamiza
taifa.
Ni uthibitisho tosha kwamba hawa ndiyo wanaowahonga
wanachama wa Chadema na watu wengine ili watoe ushahidi feki dhidi ya Lwakatare,
na kwamba ni usalama wa taifa walioandaa ile video uchwara inayopigiwa chapuo na
Mwigulu.
Ndugu waandishi wa habari;
Chama Cha Mapinduzi
kinajua kwa hali ya sasa hakiwezi kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 huku Chadema
ikiwa katika hali nzuri ya kisiasa tunayoiona sasa. Wanajua kabisa CCM
imegawanyika, kundi lolote litakalopita ndani ya CCM, litahujumu kundi jingine.
Ni kama ilivyotokea uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki.
Ndiyo maana wanapanga kila mbinu kutaka kuiangamiza
Chadema. Nasi tunasema katu hatutakubali kuona Chadema kinakufa. Tutapambana
usiku na mchana. Juna na mvua. Hadi tushinde hila hizi.Tunawaambia wanachama
wetu na wale wanaotuunga mkono, Chadema ni chama kikubwa. Kina mtandao kila
mahali, kuanzia Ikulu hadi polisi; na hivyo hakitakufa au kuzorota kwa mambo ya
kupikwa.
Ni imani yangu kwamba amri ya mahakama itawafichua
wote hawa ni kuirudisha Tanzania katika amani yake. Ni lazima tufikike mahala
watu hawa wafahamike mbele ya umma, tunataka wafahamu kuwa maisha ya mwanadamu
yana thamani kuliko siasa chafu na ufisadi wanaouendeleza.
Nawashukuru kwa kunisikiliza.
Mabere
Marando,
Dar es
Salaam
Post a Comment