JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA
TANZANIA
Taarifa kwa Vyombo vya
Habari
14 Aprili, 2013
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
linasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu)
ambaye amefariki dunia tarehe 14 Aprili, 2013 saa kumi na mbili na nusu
asubuhi, katika Hosptali ya TMJ.
Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika Jeshini
na Serikalini, Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) alikuwa Mkuu wa
JKT wa tano. Kama mnavyofahamu umuhimu wa JKT, yeye ni miongoni mwa Makamanda
walioleta tija kubwa katika kuwalea Vijana wa Kitanzania na kuwajengea nidhamu
na uzalendo.
Mpango wa Mazishi unafanywa, mtajulishwa baadae juu ya
wapi na lini atazikwa Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (Mstaafu). Msiba
upo nyumbani kwake Mikocheni, karibu na nyumbani kwa Hayati Mwl J.K
Nyerere.
MUNGU
AILAZE MAHALI PEMA PEPONI
ROHO
YA MAREHEMU
Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (MSTAAFU)
AMINA.
Imetolewa
na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Post a Comment