TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI KUTOKA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA
ARUSHA
TUKIO LA MAUAJI
MNAMO TAREHE 09/04/2013 MUDA WA SAA 2:30 USIKU HUKO LEMARA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JUMA S/O RASHID (45) MFANYABIASHARA WA MADINI NA NI MKAZI WA SOMBETINI, ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GEORGE KARAU MARRIE (38) MFANYABIASHARA NA NI MKAZI WA LEMARA.
UCHUNGUZI WA AWALI ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA ULIBAINI KWAMBA, MAREHEMU JUMA S/O RASHID, FRANCIS S/O EDWARD (37) NA MTUHUMIWA GEORGE KARAU MARRIE WALIKUWA NI WASHIRIKI KATIKA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE.
INASEMEKANA KWAMBA BAADAE WALIINGIA MAKUBALIANO AMBAPO MTUHUMIWA ALIKABIDHIWA MADINI AMBAYE THAMANI YAKE BADO HAIJAJULIKANA NA FRANCIS S/O EDWARD PAMOJA NA MAREHEMU ILI AKAUZE.
JUZI TAREHE 08/04/2013 MTUHUMIWA GEORGE S/O KARAU MARRIE ALIWASILIANA NA MAREHEMU PAMOJA NA FRANCIS S/O EDWARD NA KUWAAHIDI KUWALIPA FEDHA ZAO SIKU YA TAREHE 09/04/2013.
TAREHE 09/04/2013 MUDA WA SAA 2:15 USIKU, MAREHEMU PAMOJA NA MWENZAKE FRANCIS S/O EDWARD MWASHUYA WAKIWA NA GARI AINA YA HONDA LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 230 CBE WALITOKA MAENEO YA MJINI NA KUELEKEA MAENEO YA LEMARA. WALIPOKUWA NJIANI WALIKUTANA NA MTUHUMIWA AMBAYE ALIPANDA GARI HILO HILO NA KUKAA KITI CHA NYUMA NA MAREHEMU ALIKUWA ANAENDESHA GARI HUKU MWENZAKE AKIWA AMEKAA KITI CHA MBELE CHA UPANDE WA KUSHOTO. WOTE WALIKUWA WANAELEKEA LEMARA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA ILI AKAWAPATIE FEDHA AMBAZO ALIKUWA ANADAIWA.
WALIPOFIKA ENEO LA TUKIO, MTUHUMIWA ALIAMURU GARI HILO LISIMAME NA KISHA AKATOA BASTOLA NA KUMPIGA MAREHEMU SEHEMU YA KIFUANI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA KISHA KUMJERUHI KWA RISASI FRANCIS S/O EDWARD MWASHUYA SEHEMU YA KICHWANI.
MARA BAADA YA MAUAJI HAYO, MTUHUMIWA ALIMPORA FRANSCIS S/O EDWARD FEDHA TASLIMU TSH 400,000/=, MADINI YA TANZANITE AMBAYO THAMANI YAKE BADO HAIJAJULIKANA NA KISHA KUCHUKUA HATI YA NYUMBA NA KUTOKOMEA MAENEO YA LEMARA BWAWA LA MAJI MACHAFU.
KUFUATIA TAARIFA JUU YA TUKIO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIOKUWA DORIA MAENEO JIRANI WALIKWENDA KATIKA ENEO HILO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA KUFANIKIWA KUPATA MAGANDA MAWILI YA RISASI. JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA KUFANYA UPELELEZI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI CHA HOSPITALI YA MOUNT MERU KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI NA MAJERUHI AMELAZWA KATIKA HOSPITALI HIYO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HUKU HALI YAKE IKIENDELEA VIZURI.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI,
(SSP) ZUBERI MWOMBEJI
TAREHE 10/04/2013.

Post a Comment