Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) akitoa maelekezo
alipotembelea mradi wa ujenzi jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa Dodoma.
Kulia ni Katibu Tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge.
*********
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amewataka watumishi wa serikali
kutambua kuwa wanawajibu mkubwa wa kujenga taswira nzuri ya utumishi wa
umma hapa nchini kupitia utendaji uliotukuka.
Balozi Sefue alieleza hayo mwishoni mwa wiki alipokutana na watumishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ambapo alisisitiza kuwa watendaji na viongozi wote wa umma kuanzia ngazi za chini za uongozi na utumishi wanatakiwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo na kuondoa taswira mbaya inayouandama utumishi wa umma.
Kwa upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge alibainisha kuwa pamoja na tatizo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutokuwa na jrngo lake la ofisi, matatizo mengine yanayoikabili sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ni pamoja na Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha kidogo za kuendeshea ofisi wakati gharama za uendeshaji zinapanda.
Aidha uchache wa watumishi hasa
kwenye kada za afya ni tatizo linguine lenye kuhitaji utatuzi na
kumuomba katibu mkuu kiongozi kutoa vibali kwa maombi yote ya kuajiri
yatayomfikia mezani kwake na kuiomba serikali itenge bajeti ya kuajiori
watumishi wa kada zenye upungufu ili sekretarieti za Mikoa ziweze
kuajiri na kuziba nafasi wazi.
Akiwakilisha watumishi wengine, Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Hospitali
ya Mkoa wa Dodoma Dr. Lucy Mkandawile alisema kuwa matatizo mengine
yanayogusa watumishi moja kwa moja ni pamoja na uchelewaji kupanda vyeo,
malimbikizo ya Mishahara baada ya kupanda vyeo, malipo ya nauli za
likizo na matibabu, fedha kwa ajili ya sare za kazi, ufadhili wa masomo
kwa watumishi kwa ajili ya kujiendeleza na mishahara midogo.
Akijibu hoja hizo katibu Mkuu alieleza kuwa serikali inazifahamu baadhi
ya changamoto zilizoelezwa na inazichukua zote pamoja na zile mpya
zinazoendelea kuibuliwa na kuahidi kuwa serikali itaongeza jitihada
katika kuzishughulikia lengo likiwa kuzidi kuboresha mazingira ya utumishi wa umma na hali za maisha za watumishi.
Credits: Lukaza
Post a Comment