Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TIMU NNE MPYA KUINGIA KIPINDI CHA MWISHO CHA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ AFRIKA MASHARIKI

 



 Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha tano cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kutoka kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania – bluu, Uganda- kijani na nyeusi.
April 10, 2013, Dar es Salaam; Jumatano iliyopita katika sehemu ya nne kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalikuwa na ushindani mkubwa  lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya Pan- Africa, baada ya kuwapiga chini timu za Tanzania na Uganda. Katika kipindi hiki cha nne washiriki walijitahidi kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea mpira na kujipatia alama nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa ufasaha.Washiriki kutoka Kenya walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga  ukuta  wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola kimarekani  1,500. 
Enphatus na Samwel wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Washiriki bora watakwenda kukutana uso kwa uso na mashabiki wa soka kutoka nchi za Cameroon,Ghana,Tanzania, Kenya, na Uganda  ili atakayeonesha ufahamu na ujuzi zaidi wa soka atavishwa taji la ubingwa wa` Pan-African’.
 
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya  Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .
Katika kipindi cha tano cha mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana Jumatano hii.
               
Timu ya blu-Tanzania:
·         Khenry Sadallah(26) na Abubakari Mohamed(19)  kutoka Dar-es-Salaam watashiriki katika sehemu ijayo. Harry atakuwa kichwa cha timu ambaye ni mshabiki wa AC Milan wakati Abubakari  ambaye ni mwanafunzi na mshabiki wa Manchester United ataonesha  uwezo wake wa kucheza mpira
Timu nyekundu-Kenya:
·         Ken Muturi (26) na Chris Mwamgi (19) wote kutoka Nairobi wanamatumaini makubwa yakuwa timu ya mwisho kuingia kwenye mashindano ya Pan African.  Ken ni mfanyabiashara kwa njia ya mtandao, ni mpenzi wa mpira wa miguu ambapo atakuwa kichwa cha timu wakati Chris ambaye ni mchezaji wa Springland FC ataonesha kipaji chake cha mpira wa miguu.
Timu ya kijani-Uganda
·         Mfanyabiashara Ian Ford(24) na mwanafunzi wa uchumi Herbet Odipio(23) kutoka Kampala ni mashabiki wa Manchester United watashiriki katika kipindi kijacho cha mashindano Guinness Football Challenge. Ian atakuwa kichwa cha timu wakati Herbet ataonesha uwezo wake wa kusakata kabumbu.
Timu nyeusi-Uganda:
Edward Lyukamuzi(23) na Timothy Nimungu(22) kutoka Kampala ni timu ya pili kutoka Uganda watashiriki kipindi cha 5 cha mashindano haya. Edward ni mtaalamu wa Teknolojia ya mawasiliano ndiye kichwa cha timu wakati Timothy ambaye ni mtaalamu wa masoko atonesha uwezo wake wa kucheza soka.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa njia ya mtandao. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.  
Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya, Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufuatilia  ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.
Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya  Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. 
*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.  Tafadhali Kunywa kistarabu.
Note:
The GUINNESS and FOOTBALL CHALLENGE, and GUINNESS VIP words and associated logos are trade marks
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top