Na Mwandishi
wetu
Wakati timu ya netiboli
ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa Queens imeishushia kisago cha
mabao 36-2 timu ya kombaini wa walimu wa Wilaya ya Kibiti, wenzao wanaume, Taswa
FC imechapwa mabao 2-0 na timu ya kombaini ya Walimu kwa upande wa mpira wa
miguu.
Huu ni ushindi wa pili
kwa Taswa queens tokea kuanzishwa kwake April 6 mwaka huu na kuifunga timu ya
Kiliflora queens kutoka mkoani Arusha kwa mabao 28-8 katika mchezo uliofanyika
kwenye uwanja wa TCC, Chang’ombe.
Ikicheza kwa uelewano
mkubwa, Taswa Queens iliwabana wapinzani wao kila kona na kufunga mabao 18-1
hadi mapumziko. Katika mchezo huo Imani Makongoro kutoka Mwananchi
Communications Limited aliyechezea nafasi ya GA alifunga mabao 16 na Amina Mussa
wa BTL aliyechezea mafasi ya GS alifunga mabao 20.
Wachezaji wengine
waliocheza mechi hiyo ni Clensenia Tryphone (Tanzania Daima), Elizabeth Mbassa,
Sharifa Mustapha na Johari William wote wa Business Times Limited (BTL).
Kwa upande wa soka,
mabao yaliyofungwa ndani ya dakika 10 na timu ya kombaini ya
walimu, yalidumu muda wote wa mchezo na kuifanya timu hiyo kutoka uwanjani
kichwa chini. Mabao ya walimu yalifungwa na Hamidu Mwichande na Juma
Kimondoo.
Walimu walionyesha uwezo
mkubwa katika dakika 25 za mwanzo na kuifanya Taswa FC kutweta katika muda huo,
hata hivyo kibao kilibadilika na Taswa FC kutawla muda uliobaki huku ikosa
nafasi kadhaa za wazi.
Kutokana na kipigo
hicho, Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa wanajipanga kulipiza
kisasi kwa kurejea tena kucheza Kibiti. “Tumefungwa kutokana na uchovu sa
safari, tulifika saa 9.15 alasiri, tukapata chakula na kwenda moja kwa moja
uwanjani, hatukuwa wanyumbulifu, hata hivyo tunaahidi kurejea tena nakulipiza
kisasi,” alisema Majuto.
Kiongozi wa timu ya
walimu, Hamza Malwile, alisema kuwa wamefuraishwa na ujio ya waandishi na kutoa
hamasa kubwa ya michezo. Malwile ambaye ni mwenyekiti wa timu, alisema kuwa
watajipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano.
credits: Father Kidevu
Post a Comment