taarifa ambazo tunazo mpaka sasa ni kwamba madereva wa bajaji jana April 3 2013 waliamua kuvamia kituo cha polisi Kawe Dar es salaam wakitaka Mwanajeshi anaeshikiliwa na kituo hicho anaedaiwa kumuua mwenzao kwa kumpiga, aachiwe huru ili wamuadhibu wenyewe.
Taarifa ambazo bado hazijadhibitishwa na Polisi lakini zimezungumzwa na mashuhuda wengi, zimesema Mwanajeshi huyo alipanda Bajaji ya Marehemu na kudai haoni simu yake kwenye bajaji hivyo alihitaji irudishwe lakini marehemu akasema hakuona simu yoyote kitendo ambacho inadaiwa kilimfanya Mwanajeshi huyo kuwachukua wanajeshi wenzake na kumpiga marehemu kwa kisa cha wizi mpaka kufariki.
Credits: Millard Ayo
Loading...
Post a Comment