
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza ngoma ilkiyokuwa ikipigwa na
kina mama, kwenye tawi la CCM Nawenge Ulanga, alipowasili kwenye tawi hilo
kukagua uhai wa Chama, Aprili 15,
2013.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika
Kijiji cha Mwaya, Ulanga, Morogoro, Aprili 15,
2013.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa aliyekuwa
mwanachama wa chama hicho, Abeid Mloka aliyetangaza kuhamia CCM, wakati Kinana
alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji cha Mwaya, Ulanga mkoani
Morogoro, Aprili 15, 2013. Mloka alikuwa miongoni mwa vijana watano walioamua
kuahamia CCM papo hapo.

Katibu
wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib, akionyesha kadi za Chadema ambazo
vijana waliokuwa wanachama wa chama hicho waliamua kumkabidhi papo hapo, Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika
Aprili 15, 2013, kwenye Kijiji cha Mwaya, Ulanga mkoani
Morogoro.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Pancras Mogela aliyekuwa mwanachama wa
Chadema akipoamua kujiunbga na CCM, Kinana alipotembelea tawi la CCM Viwanjani,
Ulanga mkoani Morogoro, kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013.
Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif
Khatib.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa Nahodha wa timu ya
Libenenga, Steven Maundu, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwa kuibugiza timu
ya Nkongo mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kinana CUP, kwenye Uwanja wa
Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Pamoja na zawadi hiyo, ameipatia
timu hiyo zawadi ya sh. 100,000 kiasi kinacholingana na alichoipa timu
iliyofungwa. Kulia ni Nahodha wa timu ya Nkongo, Abdallah
Mazengo.

Mwenyekiti
wa CCM shina la Mawasiliano, Ulanga, mkoani Morogoro, Petro Kabisi
akiwatambulisha viongozi wa shina hilo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana aliyetembelea tawi hilo kukagua uhai wa Chama, Aprili 15,
2013.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitia saini kitabu wageni alipokagua uhai wa
Chama kwenye tawi la CCM la Ulanga mjini,mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013.
Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohammed Seif
Khatib.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa Magdalena Mashinga,
alimkabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya kwenye tawi la CCM la Mawasiliano,
wilayani Ulanga,Aprili 15, 2013, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama
mkoani Morogoro. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib
na Mwenyekiti wa CCM mkoa hu, Innocent
Edward.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Katibu wa tawi la CCM
Kiwanjani, Ulanga,mkoani Morogoro, Francis Kanyali aliyekuwa akisoma taarifa,
Kinana alipotemebea tawi hilo kukagua uhai wa Chama, Aprili 15,
2013.

Katibu
wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib akikagua daftari la wanachama wa CCM
kwenye tawi la Mawasiliano, Ulanga mkoani Morogoro, alipofika hapo na Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Aprili 15,
2013.

Wananchi
wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara
wa CCM uliofanyika Aprilki 15, 2013 kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani
Morogoro.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
CCM tawi la Ulanga Mjini mkoani Morogoro, baada ya kukagua uhai wa Chama kwenye
tawi hilo, Aprili 15, 2013.Picha na Bashir
Nkoromo


Post a Comment