Leo ilikuwa ni siku ya uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katiba ngazi ya Mtaa ambapo Dar ilifanyika leo na huo ni sehemu mojawapo ya Wakaazi wa Mtaa waliojitokeza kwenye uchaguzi huu ambao niliushuhudia na kushiriki kikamilifu.
Mmojawapo wa Wagombea, Abdulhaman Kasim Ngamba akinadi sera zake ambapo mwisho wa siku aliibuka mshindi wa kwanza wa jumla kwa kundi la vijana na kwa washiriki wote.
Mgombea mwingine Marry Chilala akinadi sera zake kwa Wananchi ambapo naye pia aliibuka mshindi wa pili wa ujumla na mshindi wa kwanza kwa upande wa kundi la Wanawake.
Mgombea mwingine Emmanuel John akinadi sera zake kwa umma ambapo naye pia aliibuka mshindi wa pili kwa upande wa kundi la vijana na mshindi wa tatu kwa makundi yote. Kijana yupo safi.
Mgombea Emmanuel John akipiga kura
Ulifika wakati wa zoezi zima la kuhesabu kura ukawadia
Hapa Emmanuel John akitangazwa Mshindi wa Mjumbe wa Baraza la Katiba Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutokana na uamuzi wa kura za Wananchi.
Kuja jamaa alipanda jukwaani kuja kumpongeza Emmanuel John kwa ushindi alioupata.
Mtu wa watu, Emmanuel John akipongezwa na Wananchi kwa ushindi wa kishindo aliouvuna
Kadri muda ulivyozidi kusonga kila mdau alikuwa na hamu ya kupiga picha na Emmanuel John.
Wakazi waliojitoza kwenye zoezi zima la uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katiba Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Post a Comment