![](http://2.bp.blogspot.com/-LLLBdDXILXU/UHFGDqKLsHI/AAAAAAAAN4c/OwPBeC56oCE/s320/KIKWETE.jpg)
Najua unaweza ukashtuka lakini
hautakiwi kupepesuka kwani umefika wakati kwa Wananchi kuweza kuambiwa ukweli
dhidi ya Viongozi wao, kuambiwa ukweli dhidi ya matendo na hali za viongozi wao
zilivyo kabla na baada ya kuingia madarakani.
Kwa wale wenye kumbukumbu sawia
watakumbuka kuwa mwishoni mwa Mwaka jana zilitolewa tafiti mbalimbali za hali
za kiuchumi za Wanasiasa na Wafanyabiashara. Mathalani tulipashwa kuwa Mnigeria Aliko Dangote ndiye kinara wa
utajiri Afrika, huku akishika nafasi ya 76 kwa utajiri duniani kwa mujibu wa
Jarida maarufu la Forbes, toleo lake la mwaka 2012.
Aliko Dangote mwenye utajiri wa
dola za Marekani wa bilioni 11.2 za Kimarekani (Sh trilioni 18).
Mbali ya kuongoza Afrika, duniani ni tajiri wa 76 kati ya mabilioni 1,226
wanaotambuliwa kote duniani.
Halikadhalika tuliambiwa nchi za
Afrika Mashariki nazo zina mbabe wake mwenye nguvu kubwa kiuchumi.Ndiye
anayeongoza katika `ligi’ ya utajiri wa fedha kwa nchi kadhaa za Kusini mwa
Jangwa la Sahara, zikiwemo Tanzania, Uganda na nchi jirani za Rwanda, Burundi,
Msumbuji na hata Zambia.
Jarida maarufu la Forbes, toleo
lake la mwaka 2012 linamtaja mbabe huyo kuwa ni Uhuru Muigai Kenyatta, mmoja wa
mawaziri vijana wa Kenya.
Uhuru anatajwa kuwa ndiye mtu
tajiri zaidi kuliko wote katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Kwa Afrika, Uhuru anashika nafasi
ya 26, lakini kwa Kenya na Afrika Mashariki, ndiye kinara kutokana na kuwa na
utajiri unaokadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 500 (Sh
bilioni 800 za Tanzania).
Mfanyabiashara huyo aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanzisha biashara zake. Alianza kuuza urojo Zanzibar na baadaye alifungua mgahawa miaka ya 1970.
Mgahawa huo ulipanuka na alitumia faida yake kufungua mashine ya kusaga pamoja kiwanda za usindikaji vyakula, huku akiunda Kundi la Makampuni ya Bakhressa.
Aliendelea kusindika vyakula mbalimbali na kutengeneza unga wa mahindi na baadaye kuanzisha kiwanda cha kuoka mikate na baadaye kutengeneza chocolate, ice cream, vinywaji na makasha ya kufungashia bidhaa. Kutokana na shughuli hizo, kwa mwaka huingiza Sh800 milioni.
Uhuru Kenyatta ni mmoja
wa watu wawili tu wa Afrika Mashariki waliomo orodha ya mabilionea 40
wanaotambuliwa barani Afrika.
Mwingine, Chris Kirubi pia raia wa
Kenya, ndiye anayeshika nafasi ya pili kwa utajiri Afrika Mashariki, wakati
barani Afrika anashika nafasi ya 31.
Akiwa na umri wa miaka 70,
amefanikiwa kukusanya utajiri wa dola milioni 300, sawa na Sh bilioni 480 za
Tanzania! Uhuru, mtoto wa kwanza wa Jomo Kenyatta, ana utitiri wa biashara na
ardhi ya kutosha ndani ya Kenya.
Anatajwa kuwa na zaidi ya ekari
500,000 ndani ya Kenya, akirithi ardhi iliyotwaliwa na baba yake katika miaka
ya 1960 na 1970.
Anamiliki kiwanda kikubwa cha
bidhaa za maziwa cha Brookside Dairies, kituo maarufu cha televisheni cha K24,
benki na hisa katika moja ya mashirika makubwa ya ndege nchini humo, achilia
mbali biashara nyingine kubwakubwa za ndani na nje ya Kenya.
Wakati Wakenya hao wakichomoza
katika orodha ya matajiri 40 wa Afrika, Tanzania haina hata bilionea mmoja.
Kama hiyo haitoshi, pia
tulisikia kutajwa kwa Wafanyabiashara watano Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam
Aziz, Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wakitajwa na Jarida la Ventures Africa
linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri
zaidi nchini.
Kwa mujibu wa gazeti la
Mwananchi lililotoka mwishoni mwa Mwaka jana lilieleza vizuri kuwa “anayeongoza
katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola
za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na
Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi
cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420
milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni -
Dola 110 milioni).
Kwa upande wa Said Salim
Bakhresa Jarida hilo lilisema chanzo cha utajiri wa Bakhressa ni mapato
yanayotokanana uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye viwanda vyake.
Mfanyabiashara huyo aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanzisha biashara zake. Alianza kuuza urojo Zanzibar na baadaye alifungua mgahawa miaka ya 1970.
Mgahawa huo ulipanuka na alitumia faida yake kufungua mashine ya kusaga pamoja kiwanda za usindikaji vyakula, huku akiunda Kundi la Makampuni ya Bakhressa.
Aliendelea kusindika vyakula mbalimbali na kutengeneza unga wa mahindi na baadaye kuanzisha kiwanda cha kuoka mikate na baadaye kutengeneza chocolate, ice cream, vinywaji na makasha ya kufungashia bidhaa. Kutokana na shughuli hizo, kwa mwaka huingiza Sh800 milioni.
Kampuni zake kwa sasa zinafanya
biashara mbalimbail katika nchi za Tanzania, Uganda, Malawi, Rwanda na Msumbiji
na ameajiri zaidi ya wafanyakazi 2,000”.
Katika ripoti za tafiti zote
hatujawahi kusikia kutajwa kwa Viongozi wetu kuwamo katika makundi tajwa. Je,
ni kweli viongozi wetu tulionao ni maskini? Hawana utajiri wowote ule jamii
unaoufahamu? Je, maskini kama sisi tusiokuwa na madaraka? Je, ni maskini kama
sie tusio na ilani ya kuizungumzia?
Wakati nikiyawaza hayo nikapata
wazo la kutokuanzia mbali juu ya kufikiri dhidi ya viongozi wetu ambapo jina la
haraka haraka lililokatiza fikrani ni la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete almaarufu kama JK ambaye kwa sasa ndiye “top”
wa kimadaraka (ni Rais) na ndiye amepewa Ilani ya Uchaguzi aitekeleze huku
tukishuhudia serikali yake ikitenga Mabilioni ya mapesa kufanikisha zoezi zima
la utekelezaji wa ilani hiyo.
Kwa wale Wanaomfahamu JK hana
historia ndefu wala hana historia fupi ya Kiungozi lakini mafanikio aliyoyapata
kipindi kifupi ni makubwa kuliko historia ya maisha yake ya kisiasa. Hilo
halina ubishi.
Hapa panahitajika utulivu na
umakini mkubwa ili tupate kuyang’amua mafanikio aliyoyavuna Rais Kikwete ndani
ya kipindi kifupi kabisa cha maisha yake ya kisiasa yatakayomfanya aingie
kwenye orodha ya viongozi watakaokumbukwa na Wananchi kutokana na utajiri wa
aina yake alionao.
Kwa upande wa pili ningependa
tuyamulike maeneo machache sana ambayo yamemjengea utajiri mkubwa sana Rais
Kikwete ndani ya kipindi kifupi cha utawala wake akiwa kama Rais wa nchi.
SAFARI ZA NJE
Wakati nikiifikiria hii “point”
nikayakumbuka maeneo makuu matatu yaliyokatiza kichwani kwangu. Kwanza kabisa
nilikumba wazo aliloniandikia mmoja wa wanaoperuzi blogu yangu ya www.ndgshilatu.blogspot.com
ambapo alitoa “comment” iliyosomeka:
“Ikiwa
rais Obama alikaa madarakani kwa miaka minne na kufanya jumla ya safari 32 na
KUTAKIWA kutaja faida ya kila safari, Mw. J.K Nyerere alikaa madarakani miaka
25 na kufanya jumla ya safari 68 tu lakini kilichofanyika kilionekana
wazi(tunasikia mambo yalivyoikuwa mazuri). Ndg J.K Mrisho amekuwa madarakani
kwa muda wa miaka 7 na kufanya jumla ya safari 322(ukiondoa za hivi karibun)”.
Mwisho wa kunukuu.
Hayo
ni mawazo ya msomaji wangu wa Blogu aliyaandika ambapo kwa wakati huu
nimeyakumbuka ingawaje sina hakika na takwimu zake bali naishia kuyaheshimu
mawazo yake.
|
Jambo ama tukio la pili
nililolikumbuka ni lile Sakata la Kigogo wa Ikulu ambaye alihusishwa na njama za kutaka kuchota
kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais baada ya suala hilo
kulipuka kwenye kamati mojawapo ya Bunge. Ni mambo makubwa haya ila yatupasa ya
Ngoswe tuwaachie wenyewe.
Eneo la tatu ambalo ningependa
tuliangalie ni kwenye uhalisia wa safari za nje zinazofanywa na Rais Kikwete
kwa kuangalia matokeo yake kwa Taifa. Hapa tutayamulika baadhi ya safari zake
za nje na matokeo yake kwa Taifa.
Tangu aingie madarakani Rais
Kikwete amekuwa na ziara za mara kwa mara za kwenda nchini Marekani.
Inawezekana kabisa utawala wa awamu ya nne wa Rais Kikwete unaongoza kwa
kuitembelea zaidi Marekani kuliko tawala zote.
Lakini kupitia ziara zake nchini
Marekani wakati wa utawala wa Rais George W. Bush ulisaidia misaada ya
kupambana na Maleria (mfano kupatiwa madawa, chanjo na vyandarua);
halikadhalika tulipatiwa msaada wa dola za Kimarekani million 700 kupitia mfuko
wa changamoto za millennia (MCC), fedha ambazo zimesaidia ujenzi wa barabara za
Mtwara-Masasi- Tunduru- Songea hadi Mbamba Bay, na ile ya Tunduma hadi
Sumbawanga.
Pia Rais Kikwete alifanya ziara
katika nchi za Brazil na India ambapo katika ziara yake nchini India ilizaa
mradi mkubwa wa kuboresha miundombinu ya maji ndani ya jiji la Dar es Salaam
pamoja na ujenzi wa chanzo kipya cha maji katikaMto Ruvu, Bagamoyo.
Huku ziara ya rais Kikwete
nchini Brazil ndiyo iliyoiwezesha Tanzania kupata wataalamu mahiri wa utafiti
wa mafuta na gesi mradi uliyozaa ujenzi
wa visima vya gesi katika mkoa wa Mtwara uliyopelekea umeme wa uhakika kwa wana
Mtwara.
Ni safari za Rais Kikwete nchini
Korea zilileta matunda ya ujenzi wa daraja la Mto Malagarasi ambapo kwa sasa
mkoa wa Kigoma uliokuwa nyuma kimaendeleo utafunguka kwa shughuli zote za
kiuchumi zikiwamo za kiutalii ambazo zitaboresha maisha ya wana Mtwara na
kuiimarisha pato la Taifa letu.
Halikadhalika Rais Kikwete
alishafanya ziara katika nchi ya China ziara iliyopelekea kuzaa ziara kubwa na
ya kihistoria ya Rais wa China, Xi Jinping ambayo ni ziara yake ya kwanza
kuifanya Barani Afrika.
Katika ziara ya Rais Xi wa China
tulishuhudia Tanzania ikisaini mikataba mikubwa 17 ya miradi mbalimbali ya
kimaendeleo isiyokuwa hata na chembe ya masharti wala hasara bali ni faida kwa
Taifa.
Baadhi ya mikataba hiyo ni
pamoja na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo itakayokuwa ndiyo Bandari kubwa kuliko
bandari zote ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara la Afrika; ujenzi wa viwanda
vya aina mbalimbali ambapo ujenzi wote utaongeza ajira nchini.
Pia kulisainiwa mkataba wa
ushirikiano wa kitaaluma utakaowawezesha maelfu ya Watanzania kupata ufadhili
wa kusoma fani mbalimbali katika vyuo vikuuvya China. Kwa kufanya hivi, adui
“ujinga” tutazidi kumdhibiti.
Mifano ya ziara za Rais Kikwete
kimataifa na manufaa yake ipo mingi sana. Jambo la maana ni kutokuangalia wingi
wa safari zake wala skendo za kigogo wa Ikulu bali tuyapime kwa kuangalia
matunda ya ziara hizo.
Matunda ya ziara hizo ni ujenzi
wa miundombinu ambayo huimarisha ti wa mgongo wa Taifa letu kiuchumi; ziara
zake zimechochea uwekezaji katika sekta mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya
Taifa letu; zimechochea maboresho ya huduma za kijamii; zimekuwa ni chachu ya
uogezeko la utalii na watalii nchini; zimeboresha mapato yetu ya ndani.
Umefika wakati kwa watafiti
kutokuishia kutoa tafiti za utajiri wa mali na fedha za watu (wakiwamo
viongozi) bali waangalie hata na utafiti wa utajiri wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Hakuna utajiri mkubwa kwa viongozi kama wao kuwa chachu ya maendeleo kwa jamii
na Taifa kwa ujumla wake, watafiti wamulike utajiri huu pia.
…….. Itaendelea ……..
Post a Comment