Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki
akiongea na Mhe. Lv Youqing, Balozi wa China hapa nchini masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na China ikiwa ni pamoja na matarajio ya nchi hizi
mbili baada ya ziara ya Rais wa China, Xi Jinping aliyoifanya hapa nchini mwezi
Machi, 2013.
Balozi wa China hapa nchini Lv Youqing
akifafanua jambo kwa Balozi Kairuki wakati wa mazungumzo
yao.
Balozi
Kairuki na Balozi Lv Youqing wakiendelea na mazungumzo huku wajumbe waliofuatana
nao wakisikiliza. Kulia ni Bw. Medard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje kutoka Idara ya
Asia na Australasia. Wengine ni Bi. Fang Wang, Afisa katika Ubalozi wa China na
Bw. Lin Zhiyong (kushoto kwa Bi. Fang), Afisa Mkuu wa Ofisi ya Biashara na
Uchumi ya Serikali ya China hapa nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa
Post a Comment