Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT), Dk. Hamis Kibola
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi
wa huduma mpya ya kukopesha kwa ajili ya kuendeleza biashara kwa wafanyabishara
wadogo na wa kati kwa masharti nafuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano,
Daudi Mbaga na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima. (Picha na
Habari Mseto Blog)
Ofisa
Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akifafanua jambo wakati wa uzinduzi
huo.
Ofisa
Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akifafanua jambo wakati wa uzinduzi
huo.
Ofisa
Mwendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, James Washima akimkabidhi mkopo wa shis milioni 4
Mkuu wa madereva wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, Mrisho Ngongo
.
Picha ya
pamoja
Na
Mwandishi Wetu
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mwendeshaji Mfuko huo
James Washima alisema kuwa mfuko umetimiza miaka 10 ambapo imeanzisha huduma
hiyo ili kuweza kukuza uchumi kwa wananchi.
Washima
alisema kuwa waliowekeza katika mfuko wa uwekezaji wa pamoja na UTT watachukua
mikopo kwa kutumia vipande wanavyomiliki kama sehemu ya dhamana na ikiwa pamoja
kuondolewa kwa gharama za kujiunga.
vipande
katika mfuko huo kutarahisha kukopa na kupunguza gharama kuweza kujiunga katika
uwezeshwaji wa mikopo.
Alisema
kuwa waliowekeza vipande hawataweza kukopa dhamani yote iliyowekezwa katika
mfuko lengo ni kuendelea kustawisha kiuchumi kwa wananchi na kuona umhimu wa
uwekezaji katika mfuko huo.
Washima
alisema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kutoa suluhisho kwa wajasiriamali
wadogo ,mfuko wa kuweka na kukopa (SACCOS) na mwananchi mmoja moja katika
upatikanaji wa mitaji kwa kuwezesha kutekeleza miradi ya kiuchumi.
Aidha
alisema kuwa wameweka mfumo ambao utaweza kurahisisha kuwafikia wananchi wa
vijijini kuweza kukopa hata kama hawako katika mfumo wa uwekezaji wa
vipande.
Alisema
mikopo hiyo katika madaraja manne ya mtu mmoja moja,kupewa dhamana ya mtu
aliyewekeza katika mfuko huo,mkopo kwa ajili ya taasisi pamoja na mkopo wa
biashara.
Post a Comment