Chanzo cha umaskini wa wananchi husika
husababishwa na bunge bovu na
legelege ambalo kimsingi haliwezi
kusimamia serikali.
Kwa sasa bunge letu limekuwa comedy show bila kujali pesa za walipa kodi
wanazozitafuna kila siku.
Tangu bunge lianze mheshimiwa spika kwa makusudi
amekuwa akiruhusu mijadala isiyokuwa na tija bungeni na wabunge wamekuwa
wakitukanana matusi ya nguoni
Wakati leo nasikiliza bunge, Mheshimiwa mmoja
alisimama tena kwa kujiamini na kudai kuwa eti umasikini wa tanzania
unasababishwa na picha ya nyoka iliyoko katika pesa zetu....
"Tanzania ni nchi masikini
kwasababu tumeweka picha ya nyoka kwenye hela zetu".... ni kauli ya Mh
Livingstone Lusinde Mbunge wa Mtera leo bungeni.
Kauli aliyoitoa Mheshimiwa Bungeni leo haiingii
akilini hata kidogo. Labda pengine kwa sababu ya upeo wangu mdogo wa
kuelewa na kufikiri .....
Ni vigumu sana kuwashawishi wananchi na jumuia
za kimataifa kuwa umasikini na matatizo yote yanayoikabili shillingi ya
Tanzania yanasababishwa na picha za nyoka...
Baadhi ya COMEDY toka bungeni:
-Kianzishwe chuo
cha kufundisha wanaume namna ya kuwafundisha namna ya kutongoza wanawake -
Mbunge viti maalum
Chadema!
-Tanzania ni nchi masikini kwasababu
tumeweka picha ya nyoka kwenye hela zetu".. hii ni kauli ya Mh Livingstone Lusinde Mbunge wa
Mtera
-Ofisi ya Waziri Mkuu,
imeomba Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwazika viongozi wa kitaifa
watakaokufa katika mwaka wa fedha unaoanza Juni, mwaka huu.
-Bangi ihalalishwe na
kua zao la Taifa!
Post a Comment