Shrikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi watakaochezesha mechi ya
marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na Barrack Young Controllers II ya
Liberia itakayochezwa Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi wa kati ni Adelaide
Ali, mwamuzi msaidizi namba moja ni Amaldine Soulaimane wakati Ibrahim Mohame
atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni
Ansudane Soulaimane.
Kamishna wa mechi hiyo
itakayoanza saa 10.30 jioni atakuwa Abdelhamid Radwan kutoka Misri. Maofisa hao
wa mechi hiyo watafikia kwenye hoteli ya Holiday Inn.
Wakati huo huo, Barrack Young
Controllers II imewasili nchini leo (Aprili 2 mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa
ndege ya PrecisionAir ikitokea Nairobi, Kenya inapounganisha safari hiyo
inayoanzia Monrovia kupitia Accra, Ghana.
Timu hiyo iliyofia hoteli ya
Sapphire Court itafanya mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake kwa ajili ya mechi hiyo huku wapinzani wao
Azam wakiendelea kujinoa kwenye uwanja wao wa Azam Complex.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF)
Post a Comment