Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAREMBO WATAKAOWANIA TAJI LA REDD'S MISS HAI HAWA HAPA

 

 
WAREMBO 14 kutoka vitongoji vitano vya wilaya za Siha na Haiwamejitokeza kushiriki shindano la kumsaka mrembo wa Hai maarufu kama Redds miss Hai, shindano linalotarajiwa kufanyika Ijumaa katika hotel ya Snow View iliyopo Bomang’ombe wilayani Hai.
 

Muandaaji wa mashindano hayo Grace Mmary kupitia kampuni ya ulinzi ya FEM ya jijini Arusha alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamlika na tayari warembo hao wako kambini kwa muda wa wiki mbili sasa katika hotel ya Sinza B.

Alisema warembo hao wamepatikana kutoka vitongoji vya Kwa Sadala,Boma Ng’ombe,Sanya Juu ,Machame na KIA ambao wana vigezo vyote huku akitamba mwaka huu mrembo wa Tanzania atatoka katika wilaya ya Hai.

“Warembo wangu ni wazuri,warefu ,wana jiamini na wanauwezo wa kuwakilisha vyema wilaya ya Hai ,mkoa wa Kilimanjaro na hata taifa kwa kuwa tunao kina Wolper wengine hapa na kina Sepetu wapo pia “alisemaMmary.

Mmary alisema miongoni mwa warembo waliojitokeza kushiriki shindano hilo ni pamoja na mdogo wa mrembo wa zamani wa Miss Tanzania(2006)Wema Sepetu,Weru Sepetu ambaye alidai kuwa huenda akafuata nyayo za dada yake.

Aliwataja warembo watakao shiriki shindano hilo kuwa ni Sharon Abdalah,Zena Ally,Ivony Steven, na Winny Shayo ambao wanatoka Machame na Sanya juu huku akiwataja wengine kuwa ni Julieth Kimaro ,Rehema John,Mary Chemponda,Catherine Leonard na Modesta Joseph.

Mmary alisema shindano hilo litasindikizwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya Rich Mavoko pamoja na Jambo squad ambapo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Novatus Makunga na majaji watatoka
mikoa ya Arusha ,Kilimanjaro na Dar es salaam.

Kwa upande wake mwalimu wa warembo hao Evameri Gamba alisema warembo wanaendelea na mazoezi ya mwisho pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo uoteshaji wa miti pamoja na kutembelea wagonjwa katika hosptali ya wilaya ya Hai.

Shindano la urembo katika wilaya ya Hai linafanyika kwa mara ya pili sasa huku wadhamini wakiwa ni TBL kupitia kinywaji chake cha Redds,Fem Security,Bonite bottlers,Snow view hotel,Panone pamoja migodi ya
madini wa Anglo America Mining na Manga Germ.
 
FATHER KIDEVU
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top