Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la SIAG la mjini Singida, Theresia Mwakasasa akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya siku moja iliyohusu madhara ya ukeketaji na manyanyaso kwa wanawake.Wa kwanza kulia ni Agnete Strom afisa wa shirika la STORM la nchini Norway anayefuata ni Chiku Alli, afisa wa afya na masuala ya jamii katika serikali ya Norway.Wa pili kushoto ni mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Fokus la nchini Norway, Anton Popic.
Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la SIAG la mjini Singida, Hadija Juma akitoa mada yake ya utekelezaji wa shughuli ya mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji.
Afisa wa afya na masuala ya jamii katika serikali ya Norway, Chiku Alli akitoa mada yake iliyohusu elimu juu ya madhara yatokanayo na vitendo vya ukeketaji.
Afisa wa afya na masuala ya kijamii wa serikali ya Norway,Chiku Alli akichangia mada zilizokuwa zikitolewa zinazohusu madhara yatokanayo na vitendo vya ukeketaji.
Baadhi ya wanasemina ya mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hill mjini Singida.
Baadhi ya wanasemina wakicheza muziki wakati wa mapumuziko ya semina ya mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa mkoani Singida wamehimizwa kushiriki mapambano ya kutokomeza ugonjwa wa lawa lawa, ili pamoja na mambo mengine kukomesha vitendo vya ukeketaji vinavyochangia vifo kwa watoto wa kike.
Akitoa mada iliyohusu madhara mbalimbali yatokanayo na vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike wakiwemo wachanga, Afisa Afya na masuala ya kijamii katika serikali ya Norway Chiku Alli amesema mapambano dhidi ya ugonjwa wa lawa lawa, yameanza mwanzoni mwa miaka ya 1960 hadi sasa, mapambano hayo bado hayajazaa matunda mazuri.
Chiku amesema ni aibu kubwa mno mapambano hayo kuchukua muda mrefu kiasi hicho, kwa madai kwamba ni elimu, usafi na upatikanaji wa maji ya kutosha, ndio njia pekee na rahisi ya kutokomeza ugonjwa wa lawa lawa.
Akifafanua zaidi, Chiku amesema ugonjwa wa lawa lawa ambao unachangia vitendo vya ukeketaji unatokana na uchafu katika sehemu ya siri ya watoto wa kike.
Kwa hali hiyo, amesema wabunge na wawakilishi wengine wa wananchi, wakishiriki kikamilifu mapambano hayo, vitendo vya kukeketa watoto wa kike, havitafanyika kabisa na vifo vitokanayo na ukeketaji vitabaki kuwa historia.
Awali Afisa wa shirika lisilo la kiserikali la SIAG Hadija Juma, alisema kati ya mwaka 2010 hadi mwaka jana, jumla ya wanawake 36,828 waliojifungulia hospitalini waligundulika kuwa wamekeketwa.
Aidha, Hadija alisema kuwa wanaendelea kutoa elimu juu ya madhara ya ukeketaji kuanzia ngazi ya wanafunzi wa shule za msingi, wazee maarufu na wananchi kwa ujumla.
Chiku ni mzaliwa wa kijiji cha Mtinko wilaya ya Singida vijijini ambaye kwa sasa anaishi Norway baada ya kuolewa nchini humo.
Post a Comment