Siku ya Jumamosi 27.04.2013.
Wasanii pia mnakaribishwa uwanjani !
Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) wanatarajia kujumuika kwa pamoja kufanya sherehe za miaka 49 ya muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, siku ya Jumamosi ya April 27, mwaka huu. Sherehe hizo zinatarajia kufanyika mjini Kolon, Ujeruman.
Kamati ya maandalizi ya sherehe hizo, imewataka Watanzania wote na marafiki wa tanzanzania, wanaishi ndani na nje ujerumani kukutana na kujumuika kwa pamoja katika kufanikisha sherehe hizo.
Aidha Kamati hiyo imewaomba wasanii mbalimbali kujitokeza kwa wingi ili kushiriki na kutoa burudani katika sherehe hizo.
"Umoja ni Nguvu ! Utengano Ni Udhaifu" Chereko Chereko Asiye na mwana Aeleke Jiwe, Watanzania jitokezeni kwa wingi
kwa mawasiliano zaidi at kamati.utu@googlemail.com
simu +49(0)1737363422
Post a Comment