Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya
Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 na mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2013/2014 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani)
inayoongozwa na Mhe. Edward N. Lowassa (Mb.) (kulia). Kikao hicho kilifanyika
katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam tarehe 3 Aprili,
2013.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa
Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia-mstari wa kwanza), akimsikiliza
Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Uongozi wa Wizara na Kamati
ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Wengine katika
picha ni Bw. John Haule (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Rajabu Gamaha (kushoto), Naibu Katibu
Mkuu.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe.
Waziri Membe (hayupo pichani).
Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wengine wa Kamati hiyo
wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Wakurugenzi wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo
pichani).
Baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Taasisi
zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza
Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Uongozi wa Wizara na Kamati
ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
Wakurugenzi na Wajumbe wengine kutoka Idara, Vitengo
na Taasisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza
Waziri Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya uongozi wa Wizara na
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Picha Zote na Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiani wa Kimataifa
Post a Comment