Wachezaji wa Yanga wakishangilia na kumpongeza mchezaji mwenzao, Simon Msuva, baada ya kuifungia bao la pili timu hiyo katika dakika ya 19. Baada ya ushindi huo sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 52 huku wapinzani wao katika mbio hizo za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam Fc, wakiwa na Pointi 46 baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon, mchezo uliochezwa kwenye Dimba la Chamazi juzi.
Katika mchezo huo Beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul, aliumia katika dakika ya 32, na kushindwa kuendelea na mchezo jambo lililomfanya kufanyiwa mabadiliko na nafasi yake ikachukuliwa na beki mkongwe wa siku nyingi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa, aliyeingia na kuonyesha uzoefu na kuwakumbusha mashabiki kuwa angali anaweza ila ni wakati tu.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Beki Nadir Haroub 'Canavaro' katika dakika ya 4, huku bao la tatu likifungwa na Hamis Kiiza katika dakika ya 43. Katika dakika ya 28 Haruna Niyonzima, aliifunga bao ambalo lilikataliwa na mshika kibendera wa mchezo huo. Zaidi Bofya HAPA chini
Bao la Haruna Niyonzima lililokataliwa.
Didier Kavumbagu, akijikunja kuachia shuti ambalo hata hivyo halikuzaa matunda baada ya kupanguliwa na kipa wa JKT Oljoro, Lucheke Mussa (kulia).
Beki wa Yanga Juma Abdul (kushoto) akiwa kwenye benchi baada ya kuumia goti.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza kuisapoti timu yao.
Hamis Kiiza (kulia) akiwatesa beki wa Oljoro na kipa wake anayesota kujaribu kuokoa mpira huo.
Credits: SufianiMafoto.com
Post a Comment