Fina Mambo akiwa na familia yake
Baadhi
ya washukiwa ujambazi nyumbani kwa mtangazaji wa kipindi cha Makutano
cha Magic FM, Fina Mango wamekamatwa.Kwa mujibu wa Fina, majambazi hao
wapo kwenye mtandao mkubwa unaofanya vitendo hivyo jijini Dar es Salaam.
Kupitia Twitter ameeleza:
Lile
kundi la majambazi lilokua likifanya uvamizi wa nyumba zipatazo 7
(kwangu ilikua ya 4) maeneo ya Kawe hadi Mbezi, ilisemekana ni kundi la
watu 40 waliosambaa kuanzia Kawe (makao makuu) Mikocheni, Kinondoni
mpaka Mbagala, Wameanza kukamatwa.
Polisi
Kawe inashikilia watu 7 ambao walikutwa na baadhi ya vitu pamoja na
bastola 1 na Gobole 1 matching risasi zilizokutwa maeneo ya tukio.
Waliokamatwa
wanaongea na kusema kote walikopeleka mali kuviuza. Ni juhudi za
kusifiwa za mmoja wa wahanga maana aliamua kulifatilia swala.
Hili
mpaka mwisho wake baada ya kuvamiwa na risasi kupigwa ndani kwake. Kwa
ushirikiano na wasamaria wema waliotoa info pamoja na Kawe Police
wamekamatwa. Kidogo twaweza lala kwa Amani sasa.
Fina Mambo alivamiwa na majambazi wafikao wanane nyumbani kwake na kupora mali na fedha.
Yo
Post a Comment