Katibu wa CCM wilaya ya Moshi, Aluu Segamba akiongoza viongozi wengine katika ziara ya kukagua miradi ya serikali ndani ya Manispaa ya Moshi |
Waandishi wa Habari Sauda Shimbo wa TBC, Johnson Jabir wa Kili Fm na baadhi ya viongozi wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa CCM wilaya, mama Elizabeth Minde (aliyevaa suti nyeusi) |
Tunakagua miradi ya serikali |
Sehemu ya Daraja la Rau, lililoko katika manispaa ya Moshi, Mkoani Kiliamnajro lilijengwa kwa kutumia kiasi cha sh. milioni 102, likiwa limekatika kabla ya kukabidhiwa kwa wananchi wa eneo la Rau. |
Katibu wa CCM, Aluu Segamba, (aliyevalia vazi la chama) akiangalia sehemu ya Daraja la Rau lililokatika |
Na Mwandishi Wetu Moshi
CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Moshi, imelikataa daraja la manispaa iliyojengwa katika kata ya Rau mbokomu lililojengwa kwa kutumia fedha za serikali kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ujenzi wake.
Wakizungumza baada ya kukagua daraja hilo, ambalo pamoja na ujenzi wake kutokamilika na kukabidhiwa kwa wananchi, Viongozi wa CCM wilayani hapa ambao walikuwa katika ziara maalum ya kukagua miradi ya serakili iliyojengwa katika manispaa hiyo, walisema inasikitisha kuona kazi muhimu kama ujenzi wa daraja likitekelezwa kizembe.
Viongozi hao kutoka katika Kamati ya Siadsa ya Halmashauri kuu CCM wilaya ya na Sekreteriet ya Halmashauri kuu ya CCM wakiongozwa na Mjumbe wa Mkutano mkuu CCM Taifa, Aggrey Marealle, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi, Elizabeth Minden a Katibu wa CCM wilaya, Aluu Segamba wamelikataa daraja hilo kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake.
Wakiwa wameongozana na Mkadiriaji wa Gharama za ujenzi wa Manispaa , Mhandisi Charles Huka na Msaidizi wa Mchumi wa Manispaa, Evera Lyimo. Viongozi hao walisema hata kiasi cha fedha cha sh. Milioni 102, kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo lililoanza kubomoka hata kabla ya ujenzi wake kukamilika ni kidogo mno ikilinganishwa na ukubwa wa kazi.
Akizungumza na TAIFA LETU.com kuhusu tamko lao, katibu wa CCM wilaya ya Moshi, Aluu Segamba alisema kimsingi wao kama chama tawala, hawajaridhika na kiwango cha ujenzi wa daraja hilo huku akiwataka wananchi kutopitisha magari yao katika daraja hilo kwa usalama wao na kuongeza kuwa ujenzi huo unatakiwa urudiwe upya.
Alisema kuwa kilichofanyika katika daraja hilo ni uhuni mtupu na kuongeza kuwa hawatakubali kuona fehda za umma zikiteketea ovyo kutokana na uzembe wa watu wachache.
“Kimsingi hili daraja hatujaridhika na kiwango cha ujenzi wake, huu ni uhuni na kamwe kama chama tawala hatuwezi kukaa kimya huku fedha za umma zikitafunwa kizembe, utajengaje daraja kwa kutumia milioni 102? Tunawaomba wananchi wasipitishe magari hapa hadi litengezwe katika kiwango kinachoridhisha,”alisema Segamba.
Naye Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa, Aggrey Marealle alisema kuwa baada ya kufanya ziara hiyo wanatarajia watakaa na kujadili kwa kina na kasha kutuma mtaalamu wao katika miradi yote waliyokagua na kasha watatuma mapendekezo yote kwa wizara ya ujenzi.
Hata hivyo Mkadiriaji wa gharama wa ujenzi wa manispaa, Charles Huka, ambaye katika ziara hiyo alimwakilisha Mhandisi wa Manispaa, Alipoulizwa kuhusu ujenzi wa daraja hilo, alisema kuwa muda wa mkataba wa mkandarasi haujakamilika na kimsingi wao wanaridhishwa na ujenzi huo.
Huka alisema kuwa kilichotokea ni sehemu ya udongo kumeguka huku akiongeza kuwa wanachokisubiri ni muda wa mkataba wa mkandarasi huyo kukamilika ndipo watakapotoa maelezo wa nini kimefanyika ila kwa sasa wanaridhika na kiwango cha ujenzi na wana imani na mkandarasi wao.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa eneo hilo pamoja na kupongeza manispaa kwa kuwahjengea daraja katika eneo hilo, wameonesha wazi wasiwasi juu usalama wao na kuliomba serikali kuhakikisha daraja hilo halileti madhara kwao.
Wakizungumza na gazeti hili, Mchungaji Frank Machange, ambaye ni mratibu wa mazingira katikiamkaisa KKKT jimbo la Moshi na mwananchi Emmanuel Erick walisema kitendo cha kujengewa daraja katika eneo hilo ni la kupongeza lakini kuna hali ya hatari kutokana na daraja kuanza kumeguka.
Miradi mingine iliyokaguliwa na Viongozi wa CCM katika ziara hiyo ni, Ujenzi wa Nyumba za walimu katika shule ya msingi Msandaka, shule ya sekondari mji mpya, Maabara ya Shule ya secondari Rau, madarasa manne Moshi Technical, Majengo ya Hospitali ya Pasua na Sehemu ya barabara ya Mwamedi Sadiki, inayounganisha kata ya Boma mbuzi na Majengo mapya.
Akitoa maelezo ya barabara hiyo, Mwenyekiti wa Mtaa, kata ya Majengo Mapya, Beatrice Kimambo alisema kuwa barabara hiyo ambayo alidai baada ya kuona ujenzi wake haukidhi viwango yeye pamoja na viongozi wenzake katika ODC walimuuliza diwani wao lakini walijibiwa kwamba swala la barabara hiyo haliwahusu.
Wanaolalamikia katika ubadhirifu wa ujenzi wa mifereji katika barabara hilo ni Meya wa Moshi ambaye ndiye diwani wa kata ya Boma mbuzi, Japhary Michael na Diwani wa Majengo Mapya, Charles Makarakara.
Kimambo aliwaeleza viongozi hao kwamba katika kufuatilia gharama zilizotumika katika ujenzi wa kingo za miferuji katika barabara hiyo ambayo mwaka mmoja tuu tangu ijengwe imeanza kubomoka, waliambiwa na diwani wao kuwa ni bilioni moja.
Post a Comment