Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Kikwete atembelea Viwanda vya BIDCO Oil na AZAM Buguruni

 


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na wadau wa lishe bora kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa wakizindua mpango wa kuweka virutubisho vya lishe bora katika bidhaa za unga na mafuta nchini uliofanyika katika kiwanda cha BIDCO Oil and Soap kilichopo katika eneo la viwanda la Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mafuta yaliyowekwa virutubisho vya lishe bora wakati alipokitembelea kiwanda cha BIDC Oil and Soap kilichopo eneo la viwanda la Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akongea na wafanyakazi wa kiwanda cha BIDCO Oil and Soap muda mfupi baada ya kuzindua mpango wa kuweka virutubisho bora vya lishe katika bidhaa za unga na mafuta uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mtaalamu wa kusaga unga Bwana Patrick Muriuki(kulia) akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuweka virutubisho vya lishe bora katika unga kwa kutumia teknolojia ya kisasa wakati Rais alipotembelea Kiwanda cha Azam kinachomilikiwa na S.S. Bhakressa Buguruni jijini Dar esSalaam kukagua uwekaji wa virutubisho vya bora katika bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo.

Rais Dkt.Jakaya kikwete akiangalia ukaguzi wa uwepo wa virutubisho vya lishe bora katika bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda cha kuzalisha unga AZAM ukifanyika katika maabara ya kiwanda hicho Buruguruni jijini Dar es Salaam leo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top