Wachezaji
wa Mchezo wa Pool,Winfrida Mponzi kutoka Chuo cha MUCCOBS na Aluiya
Herode kutoka Chuo cha SMMUCO wakishindana kulagi wakati wa mashindano
ya Safari Lager Higher Learning Pool Comitition 2013 Mkoa wa Kilimanjaro.
Mchezaji
wa Pool wa Chuo cha KCMC, Kim Kunthea akicheza dhidi ya mpinzani wake
Idrisa Juma wa Chuo cha KCMC wakati wa fainali za mashindano ya Safavri
Lager Higher Learning Pool Compitition 2013 mchezaji mmoja mmoja
(Singles) Mkoa wa Kilimanjaro.
Wachezaji wa timu ya Chuo cha Institute of Accountant of Arusha (IAA) wakishangilia na kitita cha sh.500,000/= ikiwa ni zawadi mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Lager Higher Learning Pool Compitition 2013 Mkoa wa Arusha.
*************************************
*************************************
MABINGWA
watetezi wa Mkoa wa Kilimanjaro wa mashindano ya Pool,Chuo kikuu cha
MUCCOBS, juzi walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa wa mashindano ya
mchezo wa pool kwa wanafunzi wa elimu ya juu mkoani Kilimanjaro
yajulikanayo kama 'Safari Lager Higher Learning Competition 2013'
baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Chuo kikuu cha MWENGE
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mambuo mwishoni mwa wiki.
Mashindano
hayo yaliyoshirikisha vyuo vikuu vinne vya mkoani hapo ambavyo ni
MUCCOBS,MWENGE,KCMC na SMMUCO kwa udhamini wa Kampuni ya Bia nchini
(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager.
Chuo
cha MUCCOBS kwa kutetea ubingwa huo kilijinyakulia fedha taslim
Sh.500,000 pamoja tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro katika
fainali za taifa zinazotarajiwa kufanyika Juni mosi mwaka huu jijini Dar
es Salaam.
Nafasi
ya pili ilichukuliwa na chuo cha MWENGE ambacho kilijinyakulia kitita
cha Sh.300,000.Nafasi ya tatu ilichukuliwa na chuo cha KCMC ambacho
kilizawadiwa Sh.200,000 na nafasi ya nne ni Chuo cha SMMUCO ambacho
kilipata Sh.100,000.
Kwa
upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Idrisa Juma wa KCMC aliibuka
kuwa bingwa hivyo kujinyakulia pesa taslimu Sh.150,000 pamoja na tiketi
ya kuwakilisha mkoa kwa upande wa wachezaji mmoja mmoja.Nafasi ya pili
ilichukuliwa na Kim Kunthea wa KCMC ambaye alizawadiwa Sh.100,000.
Na
kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Winfrida Mponzi wa
MUCCOBS alitwaa ubingwa huo na kuzawadiwa pesa taslim sh.100,000 pamoja
na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika mashindano ya kitaifa.Nafasi ya
pili ilichukuliwa na Aluiya Herode wa chuo cha SMMUCO ambaye alizawadiwa
pesa taslim Sh 50,000.
Wakati
jijini Arusha Mabingwa watetezi, IAA walifanikiwa kutetea ubingwa wao
wa Mkoa dhidi ya Chuo cha SILA, na kwa nafasi hiyo IAA ilijinyakulia
kitita cha Shilingi 500,000 pamoja na tiketi ya kushiliki mashindano ya
kitaifa . huku nafasi ya pili ikishikiliwa na SILA ambao walijinyakulia kitita cha Shilingi 300,000.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na CDTI ambao walizawadiwa pesa taslimu sh.200,000.
Upande
wa wachezaji mmoja mmoja wanaume Bingwa mtetezi wa Mkoa,Baraka Shayo
alitetea ubingwa wake dhidi ya Baraka Robert wa chuo cha SILA, na kwa
ubingwa huo, Baraka alijinyakulia pesa taslimu sh.150,000/= na nafasi ya
pili ilichukuliwa na Baraka Robert wa SSILA ambaye alizawadiwa
sh.100,000.
Credits: Mafoto
Post a Comment