MBUNGE
wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (pichani), amesema hana shaka na
umaarufu wake Monduli wala Tanzania kwa ujumla.
Kauli
hiyo aliitoa jana wakati akifungua kampeni za udiwani wa Kata ya Makuyuni huku
akikishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kupeleka mgombea
wake katika Kata hiyo.
“Eti
hawa wanathubutu kujinadi na kujigamba kushinda udiwani Monduli ya Lowassa
wakisema watapata kura kwa asilimia 90 jamani haya ni kweli?,” alihoji Lowassa
na kuongeza:
“Ndugu zangu sina shaka na umaarufu wangu Monduli wala
Tanzania.”
Katika mkutano huo, aliwaambia wananchi kwamba anahitaji kuona
wakikiadhibu CHADEMA kwa kukipa pigo ambalo hawajawahi kulipata mahali popote
nchini.
“Ndugu zangu atakayewapa kura hawa CHADEMA wana wa Makuyuni
atakuwa amenichoma kisu mimi, naomba msiwape kura hata moja, naomba muwafundishe
adabu,” alisema Lowassa.
Akikishambulia chama hicho kwa kutumia helikopta
katika Kata hiyo, alisema siku zote vita vya kiafrika vinapiganwa kwa kutumia
askari wa miguu na si helikopita.
Alisema CCM inatumia askari wa miguu
kuhakikisha inashinda vita vyake, hivyo haitatishika na helikopita
hiyo.
Alikirushia kombora chama hicho kwa kukitaka kisimame hadharani na
kujipapanua kama hakihusiki na vurugu zinazoendelea nchini.
Alisema kama
kweli hakihusiki na vurugu zilizopo nchini basi viongozi hao wanapaswa kujihoji
ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki.
“Nawaomba hawa CHADEMA wajihoji
ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki na vurugu hizi, je wanaifanyia nchi
yetu mema au mabaya,” alihoji Lowassa.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
-
Jioni5 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment