Mmoja wa askari wa JWTZ akipendisha bendera ya Umoja wa
Mataifa kama ishara ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja huo wanaolinda Amani katika
nchi mbalimbali za Afrika.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel
Nchimbi akiwasili kwenye Mnara wa Mashujaa viwanja vya Mnazi Mmoja katika
maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa
yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi
mbalimbali pamoja viongozi wa dini. (Picha na Dewji Blog).
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini
Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiwasili kwenye viwanja hivyo jijini Dar es
Salaam kushiriki kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa
Umoja wa Mataifa.
Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel
Nchimbi, Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw.
Richard Ragan na Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
wakitoa heshima kwa wimbo wa mataifa kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel
Nchimbi akielekea kuweka shada la maua kwenye Mnara wa Mashujaa ikiwa ni ishara
ya kuwakumbuka askari wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa walipoteza maisha
wakiwa kazini.
Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua kwenye
Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa
maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa mataifa
walipoteza maisha wakiwa kazini.
Mgeni rasmi Mh. Dk.
Emmanuel Nchimbi akitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara
huo.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini
Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akielekea kuweka shada la maua kwenye
maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa
yaliyofanyika leo kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini
Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiweka shada la maua kwenye mnara
huo.
Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa kwa niaba ya
Meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka
Askari wa kulinda Amani wa Umoja wa mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja leo.
Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) akitoa heshima zake mara baada ya kuweka shada la maua.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel
Nchimbi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya kuwakumba Askari
wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini
Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Kazi wa Umoja
wa Mataifa hapa nchini Dk. Alberic Kacou kwenye maadhimisho ya Siku ya
kumbukumbu ya Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani yaliyofanyika jijini
Dar es Salaam leo.
Zainab Abdallah moja ya Vilabu vya Umoja wa Mataifa
akighani shairi wakati wa maadhimisho hayo.
Baadhi ya Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani
wakati wa maadhimisho hayo.
Mkuu wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa
Mataifa Tanazania Bw.George Otoo (wa pili kulia) na Afisa Mawasiliano wa Umoja
wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu (kulia) wakiwa na baadhi ya maafisa mbalimbali wa
jeshi la Tanzania wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho
hayo.
Kushoto ni Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) na baadhi ya mabalozi na maafisa mbalimbali wa jeshi
nchini.
Baadhi ya Askari Wanawake wa Vikosi vya Kulinda Usalama
wa Tanzania wakiimba wimbo maalum wa kuhamasisha Amani katika maadhimisho
hayo.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk.
Emmanuel Nchimbi akipeana mikono na Askari Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani
kutoka Tanzania kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
leo.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini
Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akisalimiana na Askari wa Kulinda wa Umoja wa
Mataifa waliohudhuria maadhisho hayo leo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani kutoka
Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wananchi wakitazama yaliyokuwa yakiendelea wakati wa
maadhimisho ya kumbukumbu ya askari wa kulinda usalama wa Umoja wa Mataifa
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce
Temu akibadilishana mawazo na mmoja wa askari wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa vya
kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.
--
Na Mwandishi wetu.
Tanzania imesema shughuli ya operesheni za kulinda
amani katika mataifa yenye mvutano wa kivita barani Afrika zinakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo upelekwaji wa wanajeshi na udhibiti wa rasilimali
na utoaji wa maamuzi.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya
Kuwakumbuka Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar e s Salaam, Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh.
Emmanuel Nchimbi amesema tunapoadhimisha siku hii pia tunawakumbuka raia, askari
na wapiganaji zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha tangu mwaka 1948 wakiwa katika
zoezi la kulinda amani.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini
Tanzania Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa Bw. Alberic Kacou amepongeza vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania na
Polisi wa Usalama wa Raia kwa kuandaa tukio hilo la kumbukumbu ya walinda amani
wa Umoja wa mataifa wake kwa waume waliopoteza maisha yao.
Amesema katika siku hii ya kimataifa, tuitumie
kuwakumbuka walinda amani zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha na kuwaunga mkono
askari zaidi ya 111,000 waliopo na wanaoendelea kulinda amani katika nchi
mbalimbali zilizo na migogoro.
Post a Comment