WAZIRI Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, amesema ni jukumu la kila Mtanzania na taasisi mbalimbali kusaidia sekta ya elimu. Akizungumza mjini hapa jana, baada ya kukabidhiwa msaada wa taa za mezani zinazotumia nishati ya jua kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi wilayani Monduli, Lowassa alisema bila kuwekeza katika elimu Taifa haliwezi kuendelea.
“Bila ya elimu huwezi kusonga mbele, hivyo ni jukumu la kila mtu kusaidia katika sekta hii ya elimu,” alisema Lowassa.
Aidha, alisema amefurahishwa na uamuzi wa Serikali wa kuongeza alama kwa watahiniwa wa kidato cha nne kutokana na matokeo mabaya mwaka huu.
“Naipongeza Serikali kwa uamuzi ule baada ya ushauri wa tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha matokeo yale, tume imetufungua macho, lakini nimefurahishwa na mwamko wa wananchi baada matokeo kutolewa, kila mtu alikasirika kweli,” alisema Lowassa.
Akizungumzia juu ya msaada huo kwa wanafunzi wa shule za msingi jimboni kwake, alisema kila jitihada inayofanywa kusaidia elimu nchini, kwake huwa ni faraja kubwa.
“Taa hizi zitawasaida sana watoto wa vijijini kule ambako hakuna umeme, pia nyumbani kwao, kwa hiyo itawasaidia watoto kujiimarisha kielimu,” alisema Lowassa.
Taa hizo za nishati ya jua zilitolewa na Kampuni ya Double Tree ambayo ina mradi wa kutoa taa 200 kila mwezi kwa ajili ya wanafunzi wa maeneo mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni hiyo, Florenso Kirambata, alisema wamepanga kutumia zaidi ya Sh milioni 100 kwa ajili ya mradi huo wa kusaidia wanafunzi.
MTANZANIA

Post a Comment