Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo
na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo www.jakayafoundation. wapka.mobi/index.html
.
Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayoinamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo www.jakayafoundation.
.
Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayoinamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
Matapeli hao wanaeleza kwamba Taasisi
hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa Mtanzania yeyotemwenye umri
kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulip a ada ya shilingi
37,000/=.BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA WALA HAIHUSIANI KWA
NAMNA YOYOTE ILE NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE TOVUTI HIYO.
Kwa taarifa hii, Benki Kuu inatoa
tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na Taasisi hiyo ya kitapeli kwa
ajili ya kupata huduma za mikopo kama ambavyo inadai.
IMETOLEWA NA
IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU
YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013
IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU
YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013
Post a Comment