Ghorofa hilo linalomikiwa na mfanyabiashara maarufu
nchini Ally Raza linabomolewa baada ya kuanguka kwa jengo pacha la aina hiyo
Machi 29 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 36, kujeruhi 18 na uharibifu wa
mali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema kuwa, notisi hiyo imeanza Mei 27 hadi
Juni 3 mwaka huu.
“Tayari tumewakabidhi NHC na Ally Raza mmiliki wa jengo
la ghorofa 16 notisi ya siku saba ya kumtaka kubomoa jengo hilo ndani ya siku
saba na asipotekeleza hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa,” alisema
Silaa.
‘‘Kwa mujibu wa sheria ya mipango miji, mmiliki halali
wa kiwanja hicho ni NHC, na wao ndiyo waliomuuzia Raza eneo hilo ili aweze
kujenga ghorofa’’ alisema.
Kwa mujibu wa Silaa, kutokana na ramani iliyotolewa na
mipango miji, maeneo yote ya Kisutu yanatakiwa kujengwa ghorofa 10 na si
vinginevyo, lakini cha kushangaza, Mhandisi kutoka Bodi ya Wahandisi, msanifu
majengo na makandarasi wameweza kusimamia ujenzi wa ghorofa 16 kinyume na
taratibu.Kwa Habari zaidi Bofya
na Endelea..........
Post a Comment