Watanzania waishio New jersey na New York tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano wenu mkubwa mlio tuonyesha katika kipindi hiki kigumu. Kwa ajili ya blog za watanzania tuliweza kufikisha habari za msiba wa marehemu Adolf aka Brian aka Thadeo Lwakajende kwa watu wengi sana kwa muda mfupi sana kuliko tulivyotegemea. Kwa ushirikiano wenu huo tuliweza kufanikiwa na kuweza kukamilisha shughuli hii kwa kipindi kifupi sana kuliko tulivyokua tunafikiria.
Adolf alipelekwa kulazwa katika nyumba yake ya milele jana Jumatano May 1st, 2013 huko katika makaburi ya Mt Pleasant, Hawthorne, NY 10532
Tunashukuru sana sana kwa ushirikiano wenu mliotuonyesha na pia niwaombe radhi wale walioniandikia lakini sikuweza kuwajibu email zao.
Asanteni sana,
Pauline
Post a Comment